Showing posts with label news. Show all posts
Showing posts with label news. Show all posts

Wednesday, 3 February 2016

Jionee hapa Mahali ilipo na muonekano wake wa sasa bastola ya dhahabu ya Muammar Gaddafi


Ni miaka minne imepita toka auwawe aliyekuwa Rais wa Libya kanali Muammar Gaddafi na vikundi vya waasi wa nchi hiyo, Gaddafi alikuwa kiongozi ambaye ana miliki vitu vya thamani kubwa kama gari la kifahari lakini alikuwa ana miliki Bastola iliyopambwa kwa dhahabu.

Thursday, 21 January 2016

Rais Magufuli ameendelea kufanya uteuzi katika sekta mbalimbali,Na huu ndio uteuzi mpya alioufanya leo.


Alhamisi January 21 2016 ni siku nyingine ambayo Rais Magufuli kaendelea na moja ya majukumu yake kama Rais wa nchi, jukumu la leo ni kwamba kaendelea na uteuzi wa viongozi kwenye nafasi mbalimbali, uteuzi wa leo imelirudisha pia jina la Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Mzee Jakaya Mrisho Kikwete.

Sunday, 4 October 2015

Ujumbe wa Rais wa Marekani Barack Obama baada ya miaka 23 ya ndoa yao


October 3, 1992 Rais wa Marekani Barack Obama na mke wake Michelle walifunga ndoa katika kanisa la Trinity United Church huko Chicago. Marekani.

HICHI NDICHO ALICHOKISEMA MCHUNGAJI MTIKILA SIKU MOJA KABLA YA KIFO CHAKE..


MWENYEKITI wa chama cha DP Mch. Christoper Mtikila siku moja kabla ya kifo chake aliwataka wakazi wa mkoa wa Njombe kuto chagua rais baada ya kuingia katika chuma cha Uchaguzi Octaba 25 mwaka huu kwa kuwa yeye wagombea uraisi wote walio simamishwa na vyama vingine hapa nchini anaona wanadosari.

Wednesday, 3 June 2015

MSICHANA ALIYETOKWA NA MACHOZI BAADA YA KUMWONA RAIS KENYATTA LEO KAKARIBISHWA KABISA IKULU.


TZA MWANAFUNZI ALIYELIA KWA KUMUONA RAIS APATA FURSA KUKETI HIKULUNI 2
Mara ya kwanza msichana huyu jina na picha yake viliingia kwenye Headlines baada ya kuonekana akisalimiana na Rais Kenyatta huku akitokwa machozi.. Kumbe ni RaisKenyatta aliyemwona msichana huyo akitokwa machozi huku akimpungia mkono.. akasimamisha msafara wake na kumsalimia msichana huyo.

Wednesday, 18 March 2015

MAAJABU..MBUZI AZALIWA NA VICHWA VIWILI..JIONEE

DSC00655
Mbuzi mmoja katika Kijiji cha Kakanjuni Kenya amezaa mbuzi mwenye vichwa viwili vilivyoungana huku akiwa na midomo miwili, tukio hili limewashangazawengi walioshuhudia huku wengine wakihisi kwamba mbuzi huyo ni mkosi.

Tuesday, 17 March 2015

YULE MSIEMPENDA KAACHIWA HURU..SASA NGUMI ZOTE ULINGONI..

cheeeUnakumbuka ile skendo iliyompata bondia wa ngumi nchini Francis Cheka baada ya kumpiga na kumuumiza meneja wa baa yake akimtuhumu kusababisha hasara?

Thursday, 5 March 2015

MVUA YA MASAA MAWILI YALETA MAJANGA MKOANI SHINYANGA,,ZAIDI YA WATU 30 WAPOTEZA MAISHA

'Mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kiamkia leo imeuwa watu zaidi ya 50 na wengine zaidi ya 80 kujeruhiwa katika kijiji cha Mwakata kata ya Isaka wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Mvua hiyo iliyonyesha majira ya saa 4 za usiku ilidumu kwa muda wa masaa mawili ikiambatana na upepo mkali na mawe yaliyopelekea watu hao kupoteza maisha na wengine kujeruhiwa na kuharibu mazao  pamoja na miti .

Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha alifika eneo la tukio akiwa sambamba na mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya ambao wametoa pole kwa wafiwa pamoja na mikakati ya serikali kuangalia utaratibu wa kusaidia kaya zilizobakia.
Hata hivyo bado idadi kamili ya athari kwa ujumla ukiacha vifo vya watu haijatolewa.

Mi naungana na waombolezaji kuwapa pole ndugu jamaa na marafiki walioondokewa  na ndugu zao katika janga hili.'
Vua kubwa iliyonyesha usiku wa kiamkia leo imeuwa watu zaidi ya 50 na wengine zaidi ya 80 kujeruhiwa katika kijiji cha Mwakata kata ya Isaka wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Tuesday, 3 March 2015

Wimbo wa Marehemu Kapteni Komba Wamliza Rais Kikwete,Ally hassan mwinyi.

Wimbo wa John Komba aliouimba katika msiba wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere mwaka 1999, jana uliibua majonzi na kusababisha viongozi mbalimbali, akiwamo Rais Jakaya Kikwete, kutoa machozi ulipoimbwa kumuaga mbunge huyo.Wimbo huo uliobadilishwa maneno yanayohusu Mwalimu Nyerere na kuingizwa yanayomtaja mbunge huyo wa Mbinga Magharibi, mbali na Rais Kikwete ulimliza pia Rais mstaafu, Ali Hassan Mwinyi, Spika wa Bunge, Anne Makinda, Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka, Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, Yusuf Makamba na waombolezaji wengine.
Sehemu ya mashairi ya wimbo huo uliokwenda kwa jina la “Nani Yule” ulioimbwa na wanamuziki mbalimbali wa bendi nchini, na kuwatoa watu machozi iliimbwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye.
“Kapteni Komba familia yako umeiacha na nani, chama chako umekiacha na nani, nenda baba msalimie Mwalimu, mweleze hali ya Watanzania ilivyo hivi sasa, mweleze hali ya nchi yetu ilivyo hivi sasa hasa wakati huu, msalimie Mzee Kawawa Simba wa Vita”
Baadhi ya wanamuziki walioshiriki kuimba wimbo huo ni King Kiki, Mbunge wa Viti Maalumu, Martha Mlata, Jose Mara ambaye ni mwanamuziki wa bendi ya Mapacha Watatu na Luiza Mbutu wa African Stars.

Thursday, 26 February 2015

Breaking News: Chid Benzi Ahukumiwa Kifungo cha Miaka Miwili Jela au Kulipa Faini ya sh. 900,000


Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania Rashidi Abdallah Makwaro Maarufu kama (Chid Benzi) amehukumiwa kifungo cha miaka mwili jela au kulipa faini ya shingili laki tisa bada ya kupatikana na hatia ya makosa matatu ikiwemo kukutwa na dawa za kulevya aina ya heroin yenye thamani ya sh. 38,638, bangi ya sh. 1,720 na vifaa ya kuvutia dawa hizo kijiko na kigae.

Haya matano ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda. Sauti yake kutoka @PB CloudsFM

1890627_780321122049682_415026655172911331_o
DC wa Kinondoni, Paul Makonda

Power Breakfast ilikuwa hewani asubuhi ya leo February 26, mgeni rasmi ambaye alipata nafasi ya kufanya mahojiano ni Mkuu wa Wilaya Kinondoni, Paul Makonda ambaye vyombo vya habari vilikuwa na headlines nyingi kuhusu yeye tangu siku ambayo alitangazwa kuwa DC mpya wa Wilaya hiyo.

Hatimaye Kinyesi cha Mwalimu Kilichokuwa Kwenye Chumba Chake Kwa Miezi Kadhaa Chateketezwa



Manispaa ya Temeke leo imeteketeza kinyesi kilichokutwa katika chumba cha mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Kibasila Gaudensia Albert baada ya maofisa wa afya wa manispaa hiyo kuchukua hatua hiyo ili kunusuru afya za wakazi wa eneo hilo.

Waliomuiba Albino Pendo Wakamatwa Mwanza

Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo, amesema watu wote waliohusika ‘kuiba’ mtoto mwenye ulemavu wa ngozi (albino) Pendo Emmanuel (4) katika kijiji cha Ndami wilayani Kwimba, Mwanza, wamekamatwa.

Mzee Malecela amekitaka Chama cha Mapinduzi Kumchukulia hatua kali za kinidhamu Lowassa



Maneno aliyosema mwl. Nyerere kuwa IKULU sio pango la walanguzi usikimbilie kwenda IKULU ni mahali patakatifu mtu yeyote anayekimbilia IKULU bila kujiuliza mwogopeni hafai kuwa Rais. Maneno hayo ya mtu kukimbilia IKULU aliyarudia kuyasema Waziri mkuu mstafu mzee John Malecela.

Monday, 16 February 2015

Italia yawaokoa maelfu ya wahamiaji

Wahamiaji kutoka Afrika wakiwa wameokolewa na walinzi wa pwani ya Italia katika bahari ya Mediterani
Kikosi cha ulinzi wa pwani ya Italia kimesema kimewaokoa zaidi ya wahamiaji elfu mbili wakisafiri katika maboti katika bahari ya Mediterani-- katika operesheni kubwa kuliko zote kufanywa kwa wakati mmoja mpaka sasa.

Thursday, 12 February 2015

JIONEE HAPA KICHAPO KILIVYOTEMBEA KATIKA BUNGE LA AFRICA KUSINI...

Members of Julius Malema's Economic Freedom Fighters (EFF) clash with security officials after being ordered out of the chamber during President Jacob Zuma's State of the Nation address in parliament in Cape Town
Wabunge wenzake na Julius Malema wenye nguo nyekundu wakitolewa nje ya Bunge Afrika Kusini jana jioni February 12

Huyu ndo Kiongozi wa Kikundi cha Kigaidi Kinachoua Polisi na Kuiba Silaha Kwenye Vituo Nchini.....Anaitwa Kaisi Bin Abdullah


HATIMAYE kuvamiwa kwa vituo vya polisi na kuporwa silaha huku askari wake wakiuawa kikatili kumejulikana kunafanywa na nani kufuatia gazeti hili kunasa mkanda wa video wa mtu mmoja anayejiita Kaisi Bin Abdullah akijitapa kufanya hivyo kwa lengo la kukusanya silaha ili kulipa kisasi siku si nyingi!

Tuesday, 3 February 2015

Huyu ndiye aliewekewa mikono ya mtu mwingine..jionee hapa

opppMadaktari katika Chuo cha Tiba cha Amrita, Kochi huko India wamefanikiwa kufanya upasuaji wa aina yake wa kupandikiza mikono mipya kwa binadamu aliyekatika viungo hivyo.