Thomas Muller ameambiwa na mkurugenzi wa Bayern Munich, Karl-Heinz
Rummenigge kuwa kama anataka kuihama klabu hiyo na kujiunga na
Manchester United majira ya kiangazi mwaka huu atume maombi rasmi.
Kutokana
na taarifa zilizochapishwa katika magazeti ya Ujerumani, mshambuliaji
huyo anataka kujiunga na kocha Louis van Gaal, Old Trafford kwa ada ya
uhamisho ya paundi milioni 37.
Van
Gaal ndiye kocha wa kwanza kumuingiza Muller katika kikosi cha kwanza
cha Bayern msimu wa 2009-2010 na sasa anajaribu kumshawishi mshambuliaji
huyo wa Ujerumani ajiunge naye Man United.
Mkali wa mashuti: Muller, alivyowafunga Manchester City kwenye mchezo wa UEFA na ameonesha rekodi nzuri ya kufumania nyavu
Bosi mtarajiwa: Muller atajiunga na Louis van Gaal, kocha wa kwanza kumpanga katika kikosi cha kwanza cha Bayern.
Muller anatakiwa kumshawishi mkurugenzi mkuu Karl-Heinz Rummenigge ili amuuze.
Rummenigge ameliambia gazeti la Bild: ‘kama mchezaji hana furaha hapa Bayern Munich, lazima aje ofisini kwangu. Halafu tuzungumze kuhusu hilo”.
Muller
mwenye miaka 24 ameanza katika mechi 24 za Bundesliga na mechi 8 za
UEFA msimu huu, lakini amecheza kwa dakika 90 katika mechi 18 tu.
Alipoulizwa na Gazeti la Bild kuhusu kuondoka kwa mabingwa wa Bundesliga, Muller alijibu: ” Siwezi kuzungumzia, siwezi kuzungumzia. Huwa sizungumzii tetesi”.
Hali ngumu: Muller alishindwa kuisaidia Bayern Munich katika hatua ya nusu fainali ya UEFA dhidi ya Real Madrid mwezi uliopita
Picha ya kutengeneza: Jinsi Muller atakavyoonekana na jezi ya Manchester United
No comments:
Post a Comment