UONGOZI wa klabu ya Yanga SC umeitisha mkutano mkuu wa wanachama wa mabadiliko ya Katiba ili wanachama waweze kutoa maamuzi kwenye baadhi ya vipengele vilivyoongezwa kabla ya kuelekea kwenye mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa viongozi.
Tovuti ya Yanga SC imeandika kwamba, Katibu Mkuu wa klabu hiyo,
Beno Njovu amesema wamefikia kuitisha mkutano huo wa mabadiliko ya Katiba ili
wanachama wapate fursa ya kupitisha baadhi ya vipengele kabla ya kuelekea
kwenye uchaguzi mkuu.
Aidha Beno amesema wanachama wakishapitisha/kukubaliana juu ya
hivyo vipengele ndipo uoungozi utawasilisha mapendekezo hayo kwa TFF ambayo
ikishayabariki, yatapelekewa kwa Msajili nae akiyapitisha ndipo itakua tayari
ni Katiba halali ambayo itatumika kwwenye uchaguzi mkuu.
"Nawaomba wanachama wa Yanga wajitokeze kwa wingi kwenye
mkutano wa mabadiliko juni mosi 2014 ili
waweze kupitisha hivyo vipengele ambavyo vitapelekea kuwa na Katiba Mpya
itakayotumika kwa shughuli za kila siku
za klabu ya Yanga SC" aliongea Beno.
Eneo na Ukumbi utakapofanyika mkutano huo Juni Mosi 2014 utatangazwa hivi karibuni mara baada ya taratibu zote kukamilika
No comments:
Post a Comment