Thursday, 8 May 2014

RONALDO, PIRLO, INIESTA, USO KWA USO KUWANIA TUZO YA KIATU CHA DHAHABU

402133_heroakitomixnewsKWA mwaka wa pili mfululizo, mwanasoka bora wa dunia Cristiano Ronaldo ametajwa kushindania tuzo ya `kiatu cha dhahabu` ambapo atapambana na Andres Iniesta, Franck Ribery, Andrea Pirlo na Yaya Toure.

Tuoz hiyo ya kimataifa hutolewa mara moja kwa mwaka na inatolewa kwa wachezaji wenye umri zaidi ya miaka 28 ambao wamekuwa katika mafanikio binafsi mfululizo na mafanikio ya klabu zao, huku utu wao pia ukihusika. Mbali na nyota huyo wa Real Madrid, orodha ya wachezaji iliyoandaliwa ni: Thierry Henry, Iniesta, Manuel Neuer, Pirlo, Ribery, Wayne Rooney, Toure, Thiago Silva na mwanasoka wa kike kutoka Brazil Marta. Kura zitaanza kupigwa agosti 24 mwaka huu, huku sherehe za kutoa tuzo hiyo zikifanyika jumapili ya Oktoba 13 mjini Monaco. Mshindi atachaguliwa na mashabiki kupitia Tovuti ya Golden Foot au ukurasa wa facebook wa Golden Foot. Tuzo hii ilianzishwa mwaka 2003 na mshindi wa mwaka huu ataungana na wachezaji wengine waliowahi kutwaa ambao ni Roberto Baggio, Pavel Nedved, Andriy Shevchenko, Ronaldo, Alessandro Del Piero, Roberto Carlos, Ronaldinho, Francesco Totti, Ryan Giggs, Zlatan Ibrahimovic na Didier Drogba.

No comments:

Post a Comment