Monday, 14 July 2014
SCOLARI ATIMULIWA BRAZIL BAADA YA KUWA KOCHA WA KIKOSI KIBOVU ZAIDI KIHISTORIA
KOCHA Luiz Felipe Scolari amebwaga manyanga
Brazil baada ya wenyeji hao kuboronga katika
Fainali za Kombe la Dunia mwaka huu,
wakifungwa mabao 10 katika siku tano.
Brazil ilifungwa na Uholanzi mabao 3-0 katika
mchezo wa kuwania nafasi ya tatu ikitoka
kuchapwa mabao 7-1 na Ujerumani katika Nusu
Fainali Jumanne. Hata hivyo, bado
haijathibitishwa, ni vyombo vya Habari Brazil
vimeripiti amefukuzwa.
Scolari alikutana na viongozi wa Shirikisho la
Soka Brazil Jumamosi usiku baada ya kipigo
hicho, ambacho kiliwafanya wawe kikosi cha
kwanza cha Brazil daima kufungwa nyumbani
mfululizo tangu mwaka 1940.
SEHEMU YA PILI .. Kauli ya Mwisho ya Ballali Kabla ya Kifo Chake
Dar na Marekani. Gavana wa zamani wa
Benki Kuu ya Tanzania BOT), Marehemu
Daudi Ballali aliacha wasia unaotaka maiti
yake isionyeshwe hadharani atakapofariki
dunia na wala maiti yake isiletwe Tanzania
kwa ajili ya maziko.
Ballali aliyefariki Mei 16, 2008 na kuzikwa Mei
23 mwaka huohuo katika makaburi ya Gate
of Heaven, eneo la Silver Spring, Maryland
nchini Marekani alifahamu kuhusu kifo chake
wiki mbili kabla, baada ya matibabu
kushindikana.
Mwandishi wa Mwananchi aliyekuwa nchini
Marekani kwa siku kumi kufuatilia suala hilo,
alibaini kuwa kiongozi huyo alilazwa mara ya
pili katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha
George Washington, April 2008 na alirejea
nyumbani kwake, Washington DC wiki mbili
kabla ya kukutwa na mauti.
Habari kutoka ndani ya familia yake
zinasema baada ya madaktari kushindwa
kumtibu walimwambia kwamba asingeweza
kuishi kwa zaidi ya wiki mbili, hivyo
walimshauri ahamie kwenye ‘hospice’
ambayo ni nyumba maalumu ya kusubiri kifo
kwa watu ambao magonjwa yao
yameshindikana.
Hospice hutumika kwa ajili ya kuwaweka
wagonjwa wanaohitaji faraja hasa kutoka na
maumivu makali chini ya uangalizi wa
washauri na wauguzi kwa lengo la
kuwaongezea wagonjwa husika siku za
kuishi.
Baadhi ya hospice hutoa huduma za kiroho,
kijamii na kifedha na wakati mwingine
huduma hizo hutolewa kwa wagonjwa ambao
wanaugulia nyumbani. Hata hivyo, gazeti hili
lilidokezwa kwamba Ballali alikataa kwenda
kwenye nyumba hiyo na badala yake kutaka
apelekwe nyumbani kwake.
“Alikataa kwenda kwenye hospice,
aliwaambia madaktari kwamba yeye hawezi
kwenda huko ijapokuwa kuna huduma nzuri
na uangalizi wa nesi (muuguzi). Aliwaambia
kwamba nitakwenda kufia nyumbani kwangu
maana nina nyumbani kwangu,” kilisema
chanzo chetu na kuongeza:
“Aliporejeshwa nyumbani, alikuwa
anazungumza kama kawaida lakini kadri siku
zilivyosogea hali ilikuwa ikibadilika na kama
sikosei siku mbili au tatu za mwisho (za uhai
wake) alikuwa anajitambua lakini alikata
kauli, hakuwa akizungumza chochote”.
Uchunguzi wetu umebaini kuwa katika siku
hizo za mwisho za uhai wake, Ballali aliacha
maelekezo kwamba pindi atakapofariki dunia,
mwili wake usiwekwe hadharani kwa maana
ya kutazamwa na watu nje ya familia wala
kusafirishwa kuja Tanzania kwa ajili ya
maziko.
“He said, he doesn’t like to be turned into a
laughing staff (alisema asingependa
kugeuzwa kichekesho), sababu watu
wasingekuja kutoa heshima za mwisho, bali
wangekuja kumdhihaki kuangalia Ballali
aliyetuhumiwa kwa ufisadi wa EPA na siyo
Gavana,” kilisema chanzo hicho.
Full time ya Ujerumani vs Argentina, tuzo za wanasoka bora wa michuano
Baada ya mwezi mmoja hatimae michuano ya
kombe la dunia imemalizika nchini Brazil
ambapo mechi ya fainali iliwakutanisha
Ujerumani vs Argentina jijini Rio de Janeiro
kwenye uwanja wa Maracana.
Ushindi ni wa Ujerumani wa goli moja tu
lililofungwa ndani ya dakika 30 za nyongeza
baada ya full time kuwa 0-0 na mfungaji alikua
Mario Gotze aliesababisha Ujerumani kuchukua
ubingwa wake wa nne wa dunia.
Unaambiwa pia hii ni mara ya kwanza kwa
timu kutoka Ulaya kuchukua ubingwa wa dunia
kwenye ardhi ya Amerika ambapo pia kwenye
sentensi nyingine, tuzo ya mchezaji bora wa
mashindano imeenda kwa Lionel Messi,
mfungaji bora James Rodriguez, kipa bora
Manuel Neur na mwanasoka bora chipukizi wa
mashindano amechukua Paul Pogba.
MAONI
Friday, 11 July 2014
TETESI SOKA BARANI ILAYA..JUA HAPA KILA MCHEZAJI ANAENDA TIMU GANI
Kocha mpya wa Manchester United Louis van
Gaal angependa kumchukua Wesley Sneijder, 30,
kutoka Galatasaray, lakini klabu hiyo ya Uturuki
inataka pauni takriban milioni 6 (Sun), Liverpool
watamuuza Luis Suarez, 27, kwenda Barcelona
mwisho wa wiki hii, ikiwa klabu hizo
zitakubaliana ada ya pauni milioni 75 (Daily
Mirror), Lakini Arsenal wamekasirishwa kwa
sababu jaribio lao la kumchukua Alexis Sanchez,
25, kutoka Barcelona linacheleweshwa kutokana
na mkataba wa Suarez kudemadema (Daily
Express), Arsenal wanataka kulipwa pauni
milioni 6 kumuuza Mikel Arteta, 32, kwenda
Fiorentina (Times), Roma wamewapa
Manchester City hadi tarehe 21 mwezi huu
wawe wamekamilisha usajili wa beki wa kati
kutoka Morrocco Mehdi Benatia, 27, (Guardian),
Chelsea wanamsajili beki wa kulia wa Atletico
Madrid, Luis Filipe, 28, kuziba nafasi ya Ashley
Cole aliyekwenda Roma (Sun), winga kutoka
Colombia Juan Cuadrado, 27, huenda akahamia
Manchester United kutoka Fiorentina (London
Evening Standard), mshambuliaji wa Liverpool
Iago Aspas, 26, anajiandaa kuhamia Sevilla,
baada ya kushindwa kupata namba Anfield
(Daily Star), Brendan Rodgers pia anafikia kutoa
pauni milioni 10 kumchukua beki wa kushoto
wa Swansea Ben Davies, 21 (Daily Telegraph),
Manchester United, Liverpool, Chelsea na
Arsenal zitapambana kupata saini ya winga wa
Benfica Joao Filipe anayetajwa kuwa "Cristiano
Ronaldo mwingine" pamoja na kipa Joao
Virginia, wote wana umri wa miaka 15 (Daily
Express), Manchester United wanafikiria
kumsajili beki wa kushoto wa Wolfsburg na
Uswisi, Ricardo Rodriguez, 21, kuziba nafasi ya
Patrice Evra ambaye huenda akahamia
Juventus (Times), Lakini Louis van Gaal pia
huenda akamchukua beki Daley Blind, 24,
kutoka Feyenoord ikiwa Evra ataondoka
(Manchester Evening News), kiungo kutoka
Nigeria Michael Babatunde, 21, anayechezea
Volyn Lutsk nchini Ukraine, amedai kuwa
Sunderland wanataka kumsajili (Newcastle
Chronicle), Bayern Munich wamesema
wamefikia makubaliano yasiyo ya maandishi na
Atletico Madrid ya kumsajili Mario Mandzukic,
28 (Marca), mshambuliaji wa Real Madrid
Alvaro Morata huenda akajiunga na Juventus
mapema wiki ijayo (Tuttosport), na hatimaye,
kinyozi wa Alexis Sanchez amethibitisha kuwa
mchezaji huyo anahamia Arsenal! (Metro).
Share tetesi hizi na wapenzi wote wa soka.
Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Cheers!
JOSE MOURINHO KUMRUDISHA DARAJANI GWIJI WA CHELSEA DIDIER DROGBA
KLABU ya Chelsea inaangalia
uwezekano wa kumrudisha
Didier Drogba katika dimba la
Stamford Bridge.
Nyota huyo mwenye miaka 36
anazivutia klabu za Qatar,
wakati Juventus nao
wakifikiria kumnasa mkongwe
huyo anayecheza katika klabu
ya Galatasaray ya Uturuki.
Bado Jose Mourinho ana
mahusiano mazuri na Muivory
coast huyo na anavutiwa
kumrudisha kwa majukumu ya
ukocha zaidi.
Mkongwe huyu wa miaka 36
anazivutia klabu za Qatar, nao
Juventus wanaitaka saini
yake.
Klabu hizo za Qatar zinatarajia
kutoa ofa nono na mshahara
utajadiliwa, lakini unakadiriwa
kuwa paundi milioni 3 kwa
msimu baada ya makato ya
kodi.
Wazo la kurudi Chelsea
litaangaliwa zaidi na pande
zote.
Mourinho amekuwa na
mapenzi makubwa kwa Drogba
na anajua kuwa atakuwa na
msaada mkubwa katika kikosi
chake msimu ujao.
Alionesha nia hiyo hata
Galatasaray ilipokutana na
Chelsea katika michuano ya
UEFA mwezi machi mwaka huu
na alieleza kuwa Drogba
anaweza kurudi na yuko
makini kufanikisha hilo.
Drogba alishinda makombe
matatu ya ligi, makombe
manne ya FA na kombe la
UEFA akiwa katika klabu ya
Chelsea na Mourinho anataka
kutumia uzoefu wake
kuwashauri wachezaji wake
wapya.
Thursday, 10 July 2014
SIMBA SC YAFANYA KUFURU, YASAINI WATATU KWA MPIGO LEO AKIWEMO MANYIKA JR. NA BEKI LA MWADUI
SIMBA SC imesajili wachezaji wawili chupukizi
kwa ajili ya timu yake ya vijana chini ya umri wa
miaka 20, maarufu kama Simba B, akiwemo
Peter Manyika, mtoto wa kipa wa zamani wa
Yanga SC, Manyika Opeter.
Makamu Rais wa Simba SC, Geoffrey Nyange
‘Kaburu’ amesimamia zoezi hilo lililokamilika
vyema akishirikiana na Mjumbe wa Kamati ya
Usajili, Said Tuliy leo mjini Dar es Salaam.
Pamoja na kipa huyo wa timu ya taifa ya vijana
chini ya umri wa miaka 20, Simba SC pia
imemsajili kinda mwingine kutoka Mwadui ya
Shinyanga, Ibrahim Hajibu Migomba.
Kaburu maarufu kama Perez, amesema mtoto
wa Manyika amesaini miaka mitatu sawa na
Hajibu ambao wote pamoja na kusajiliwa kama
wachezaji wa Simba B, watakuwa wanakomazwa
kikosi cha kwanza.
Awali ya hapo, leo Simba SC ilimsajili kipa wa
Mtibwa Sugar ya Morogoro, Hussein Sharrif
‘Cassilas’ aliyesaini Mkataba wa miaka miwili.
Kipa huyo bora wa Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara amekuwa akiibeba Mtibwa Sugar
kwa misimu mitatu iliyopita, tangu kuondoka
kwa Shaaban Hassan Kado.
