Kenya itacheza na Stars kesho Jumanne kwenye mechi ya nusu fainali ya Chalenji kwenye Uwanja wa Kenyatta mjini Machakos.
Bunge nchini Afrika Kusini, leo
linatarajiwa kuwa na kikao maalum cha kumkumbuka Nelson Mandela, huku
viongozi duniani wakijiandaa kwa misa ya wafu itakayofanyika Jumanne.
Kikao cha leo kinafanyika mwonzoni wa wiki ya shughuli mbali mbali za kumuenzi Mandela kabla ya mazishi yake tarehe 15 Disemba.