Kwa mujibu wa Arusha yetu Blog wanasema kuwa Chatu huyo aliuwawa na wananchi mchana wa June 05 na ni baada ya kuonekana maeneo ya Sakina Arusha akiwa amefungwa kitambaa chenye maaandishi mekundu.
Wakazi wa eneo la Sakina wamepatwa na mshtuko mkubwa,kikubwa zaidi kwa Chatu huyo ni kuwa inasemekana alionekana akiingia ndani.
Mara baada ya kuonekana kwa Chatu huyo wananchi walijipanga kisha wakafanikiwa kumuua ingawa kulitokea utata baada ya Mama mwenye nyumba aliyetokea Chatu huyo kupinga kuuliwa kwa Chatu huyo,Chatu huyo aliuwawa kisha akakatwa vipande vipande.
![CHA4](http://i1.wp.com/millardayo.com/wp-content/uploads/2014/06/CHA4.jpg?resize=403%2C537)
![CHA3](http://i1.wp.com/millardayo.com/wp-content/uploads/2014/06/CHA3.jpg?resize=486%2C272)
![CHA2](http://i1.wp.com/millardayo.com/wp-content/uploads/2014/06/CHA2.jpg?resize=484%2C363)
No comments:
Post a Comment