Anakuja: Ander Herrera anaweza kuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Louis van Gaal Manchester United kwa Pauni Milioni 28.4
KIUNGO
Ander Herrera anakaribia kuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na kocha
mpya wa Manchester United ya England, Louis van Gaal kwa dau la Pauni
Milioni 28.4.
Mchezaji
huyo wa Athletico Bilbao amekuwa akitakiwa na klabu hiyo ya Ligi Kuu
England tangu msimu uliopita, lakini sasa kocha mpya wa Mashetani hao
Wekundu, Van Gaal has anaelekea kufanya kweli kumnasa nyota huyo.
WASIFU WA ANDER HERRERA
Kuzaliwa: Bilbao, Hispania, Agosti 14 1989 (Miaka 24)
USHIRIKI WA LIGI
2008-2009: Zaragoza B (mechi 10, mabao 2)
2009-2011: Zaragoza (mechi 82, mabao 6)
2011- HADI SASA: Athletico Bilbao (mechi 94, mabao 7)
TIMU ZA TAIFA
2009-2009: Hispania U20 (mechi 10, mabao 3)
2009-2011: Hispania U21 (mechi 15, mabao 4)
2012-HADI SASA: Hispania U23 (mechi 5, hajafunga bao)
No comments:
Post a Comment