Friday, 27 June 2014

MSANII HUYU WA BONGO FLEVA AAMUA KUFUNGUKA BAADA YA KUFUNGA NDOA YA KIMYA KIMYA NA SIRI KUBWA...!!

Mwanamuziki zao la nyumba ya kukuza vipaji Tanzania ‘ THT’ , Amini Mwinyimkuu
amefunguka kuwa , aliamua kufunga ndoa ya fasta ili kuuwahi mwezi mtukufu wa Ramadhani .
Mwanamuziki zao la nyumba ya kukuza vipaji Tanzania ‘THT ’ , Amini Mwinyimkuu .
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni ,
Amini ambaye amemuoa binti aitwaye Farida Bashiri alisema ilikuwa vigumu kufanya sherehe kubwa kwani lengo lilikuwa ni kumuingiza ndani haraka mke huyo ili amuandalie futari pia .
“Ni kweli nilioa juzi pale Magomeni Mwembechai , ilikuwa ni ndoa tu na niliamua kufanya hivyo ili kuuwahi mwezi Mtukufu wa Ramadhani , ” alisema Amini ambaye ndoa ilimbadili jina kwa kufungishwa kwa jina la Namini kufuata mambo ya kinyota .

No comments:

Post a Comment