MAKUBWA! Kaburi la aliyekuwa Mnajimu Mashuhuri Afrika Mashariki,
marehemu Shehe Yahya Hussein limejengwa tena baada ya hivi karibuni
kubomolewa na watu wasiojulikana, lakini sasa limedaiwa kujengwa
Kikristo na chini ya kiwango!Akizungumza na Risasi Jumamosi juzi jijini Dar, msemaji wa familia ya
Shehe Yahya, Maalim Hassan Yahya Hussein alisema kaburi hilo lipo kwenye
Makaburi ya Tambaza karibu na Hospitali ya Muhimbili, Dar sanjari na
lile la marehemu Shehe Kasim Bin Jumaa.
Alisema makaburi yote yalibomolewa wakati wa Operesheni Safisha Jiji
ambapo serikali kupitia kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck
Sadik alikataa jiji kuhusika.
Hata Maalim Hassan alikiri si serikali iliyoyabomoa makaburi hayo bali
ni wahuni wachache, lakini akasema mkuu wa mkoa aliahidi kwamba serikali
itayajenga upya tena kwa kuyaboresha.
Familia hiyo ikasema inashangazwa makaburi hayo kujengwa katika mfumo wa
makaburi ya Kikristo jambo ambalo halitoi picha nzuri kwa sababu wako
watu wanatoka nje ya nchi kuja Tanzania kutaka kuliona kaburi la Shehe
Yahya.
FAMILIA KUBOMOA
“Makaburi yale yalitakiwa kujengwa kwa kutumia kokoto maalum ziitwazo
‘mable’ na kulikuwa hakuna sababu ya kujenga ngazi ambazo watu wanaweza
kukaa kama kaburi la marehemu Steven Kanumba.
“Kama marehemu alipokuwa hai hakukaliwa kwa nini akiwa amekufa akakaliwe akiwa ndani ya kaburi? Kule ni kumkosea heshima.
“Sisi kama familia tumeamua kwamba, lazima tuyabomoe makaburi yote, la
baba na lile la marehemu Shehe Kassim siku ya Jumamosi (leo) na
kuyajenga upya tutakavyo sisi tena kwa gharama zetu, serikali ibomoe
matofali yao,” alisema Maalim Hassan.
No comments:
Post a Comment