
KLABU
ya Manchester City imefanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu soka nchini
England baada ya kufanikiwa kuwafunga West Ham mabao 2-0 katika uwanja
wa nyumbani wa Etihad.
Wanaume wa Manuel Pellegrini
walijua wazi kuwa ushindi katika mechi hiyo utawapatia ubingwa wa pili
ndani ya misimu mitatu bila kujali matokeo ya Liverpool dhidi ya
Newcastle.
Samir Nasri alikuwa wa kwanza kuifungia Man City bao la kuongoza katika dakika ya 6` tu ya mchezo huo uliovuta hisia za mashabiki wengi wa soka duniani.
Bao la pili la Man City lilifungwa dakika ya 49` kupitia kwa nahodha wake Vicent Kompany na kuihakikishia City ubingwa wa EPL.
Liverpool walitoka nyuma kwa
bao 1-0 na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Newcastle, lakini
ushindi wa Man City umewafanya washindwe kukata kiu ya kutotwaa ubingwa
kwa miaka 24, sasa imefikia 25.







Kikosi
cha Man City leo: Jart, Zabaleta, Kolarov, Toure, Kompany, Demichelis,
Silva (Milner, 76), Garcia, Dzeko (Fernandinho, 69), Aguero, Nasri.
Kikosi
cha West Ham: Adrian, O’Brien, McCartney, Taylor, Tomkins, Reid,
Downing, Noble, Carrol (Cole, 72), Nolan (Jarvis, 64), Diane (Cole, 81) .
Mwamuzi: Martin Atkinson. MATOKEO YA MECHI ZOTE EPL
Mwamuzi: Martin Atkinson. MATOKEO YA MECHI ZOTE EPL
No comments:
Post a Comment