KLABU ya Barcelona imemteua kiungo wake wa zamani, Luis Enrique kuwa kocha wake mpya.
Mwalimu
huyo mwenye umri wa miaka 44, ambaye aliiongoza Celta Vigo msimu huu,
amekubali Mkataba wa miaka miwili kurithi mikoba ya Gerardo Martino,
ambaye ameachia ngazi baada ya msimu mmoja kazini.
Klabu
hiyo ya Katalunya imesema katika taarifa yake kwamba: "Bodi ya
wakurugenzi ya FC Barcelona jioni hii imemthibitisha Luis Enrique
Martineza kuwa kocha wao mpya wa kikosi cha kwanza, kufuatia mapendekezo
ya Mkurugenzi wa Michezo, Andoni Zubizarreta. Luis Enrique, (Mwenye
miaka 44), atasaini Mkataba wa miaka miwili,".
Barcelona
pia imethibitisha kumuongezea Mkataba Leo Messi,
kumsajili kipa Marc-Andre Ter Stegen kutoka Borussia Monchengladbach na
kuwarejesha Rafa Alcantara na Gerard Deulofeu ambao walikuwa wakicheza
kwa mkopo Celta Vigo na Everton.
Kuteuliwa
kwa mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa wa Hispania ambaye alicheza
Nou Camp kuanzia mwaka 1996 hadi 2004 alipojiunga nato akitokea
wapinzani wa jade Real Madrid, ni mwanzo mpya wa kurejesha heshima ya
Barcelona iliyoshuka msimu huu.
No comments:
Post a Comment