Wednesday, 14 May 2014

FIFA YAMPA SHAVU MSEMAJI WA YANGA, YAMPELEKA SAUZ

 
Msemaji wa Yanga, Baraka Kizuguto ameula baada ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kumteua kushiriki kozi ya masuala ya uhamisho.


Kozi hiyo ya siku mbili inaanza leo nchini Afrika Kusini na itakuwa ni kujifunza kuhusiana na Mfumo wa Uhamisho kupitia mtandao (TMS) ambao unaingia katika mtindo mpya zaidi.
Kizuguto amekuwa Mtanzania pekee aliyeteuliwa kushiriki kozi hiyo nchini Afrika Kusini huku akipewa jukumu la kuwanoa wengine.
“Kweli nimepata nafasi hiyo, kawaida wanakuwa na vigezo vyao na pia wanaangalia ulifanya uhamisho mara ngapi na kwa ufanisi kiasi gani.
“Hivyo nakwenda peke yangu kutoka Tanzania na tayari nimeelezwa baada ya kurejea nitakuwa na jukumu la kuwanoa maofisa kutoka kwenye klabu nyingine,” alisema Kizuguto.
Kizuguto anatarajia kurejea nchini keshokutwa Ijumaa baada ya kozi hiyo ya uhamisho kupitia mtandao.

No comments:

Post a Comment