VAN GAAL AWAELEKEZA MAN UNITED
KOCHA wa Manchester United, Louis Van Gaal ameiagiza klabu hiyo kuelekeza nguvu katika usajili wa wachezaji wa nafasi za ulinzi na kiungo.
Wakati tetesi zinasema wamewaweka kwenye mipango ya kuwasajili Arjen Robben na Edinson Cavani, Van Gaal anatumai uhamisho wa Luke Shaw unaohitaji Pauni Milioni 27 utakamilishwa.
Pamoja na hayo, was aka vipaji wa klabu wameelekeza jicho lao katika timu ya taifa ya Uholanzi lusaka wachezaji wa kusajili.
![Potential: Bruno Martins Indi has been watched by United but Stefan de Vrij (right) is going to join Lazio](http://i.dailymail.co.uk/i/pix/2014/05/22/article-2636240-1DF46A5D00000578-491_306x423.jpg)
![Potential: Bruno Martins Indi has been watched by United but Stefan de Vrij (right) is going to join Lazio](http://i.dailymail.co.uk/i/pix/2014/05/22/article-2636240-1DF46A1900000578-370_306x423.jpg)
Wakali: Bruno Martins Indi amekuwa akifuatiliwa na United, lakini Stefan de Vrij (kulia) anaweza kuhamia Lazio
Beki wa kati wa Feyenoord, Bruno Martins Indi ni miongoni mwao, wakati mchezaji mwenzake, Daryl Janmaat, beki wa kulia pia anafuatiliwa.
Mchezaji mwenzao wa klabu, beki Stefan de Vrij amekuwa akihusishwa na Man United, lakini anaopenda zaidi kuhamia Lazio siku zijazo.
No comments:
Post a Comment