Taarifa juu ya ugomvi ulioibuka wiki
iliyopita baina ya ndugu mapacha wa kundi la P-Square Peter na Paul na
kaka zao zimewashtua mashabiki wao walioko pande mbalimbali za dunia.
Chanzo kimoja cha karibu na ndugu hao kimeelezea sababu na kile
kilichotokea.
Inadaiwa kuwa ugomvi wa wanandugu wa familia ya Okoye ulianzia kwa wasaidizi wao binafsi, ‘Personal Assistants’ (PA’s).
Ripoti kutoka katika vyanzo mbalimbali
vya Nigeria zinasema kuwa ‘PA’ wa kaka yao mkubwa Jude aitwaye Wande
alimpatia ‘PA’ wa Peter aitwaye Shege, pesa ili akamsajilie gari lake,
lakini inasemekana ‘PA’ wa Peter badala ya kutumia pesa hizo kwa kazi
aliyoelekezwa alizitumia kwa kitu tofauti.
Baada ya hapo inadaiwa kuwa ‘PA’ wa
Jude alikasirika baada ya kugundua kuwa pesa alizompa ‘PA’ wa Peter
hazikufanyiwa kazi aliyoelekeza. Alipoenda nyumbani kwa Okoye’s
‘Squareville’ ili kukabiliana na ‘PA’ wa Peter ndipo ugomvi ulizuka
baina ya wasaidizi hao wawili wa ndugu.
Chanzo kinaendelea kusema baada ya
ugomvi kuanza Peter aliingilia na kutaka kumpiga msaidizi wa Jude hadi
Paul alipoingilia kwa lengo la kuwaachanisha, lakini badala yake Peter
alijikuta akimpiga ngumi pacha wake Paul na kuanguka chini japo inadaiwa
kuwa Paul hakumrudishia ngumi kaka yake, na badala yake kaka yao
mwingine aitwaye Tony naye aliingilia na kuanza kupigana na Peter.
Wakati haya yote yanatokea mke wa Paul Anita alikuwa akishuhudia.
Chanzo kiliongeza kuwa Peter anataka
awe mhusika mkuu wa maswala ya fedha za kundi au apate mgao mkubwa
zaidi, huku upande wa pili inadaiwa Paul anataka kaka yao mkubwa ambaye
pia ni meneja wao Jude aendelee kuwa msimamizi mkuu wa maswala ya fedha
zao kama ilivyokuwa miaka yote iliyopita, lakini mpaka ilifikia hatua ya
kutaka wagawane mali kila mtu awe na chake.
Baada ya habari za ugomvi baina ya wana
ndugu hawa kuenea, hii ni post ya Paul aliyoiandika juzi kupitia
ukurasa wake wa Facebook.
“After the storm comes the calm. Hoping for better days ahead as one family. God’s intervention.”
No comments:
Post a Comment