Leo katika kipindi cha KUMEPAMBAZUKA
kinachorushwa hewani na kituo cha Radio cha RADIO ONE STERIO nimemsikia
Kamanda Aikael Freeman Mbowe akitoa ufafanuzi wa UKAWA kutoka nje ya
bunge maalumu la katiba na kutorudi tena bungeni bali kwenda kwa
wananchi.
Mheshimiwa Mbowe ameeleza jinsi ambavyo
bunge linavyoendeshwa kwa upendeleo mkubwa sana,Matusi makubwa ya nguoni
kwa wajumbe wenye mawazo tofauti na ya serikali ya ccm,kutumia vitisho
vingi,udhalilishaji na uonevu mkubwa .
Mheshimiwa Mbowe ametolea mfano kwamba
Kama Lukuvi amekwenda kanisani na kuanza kuhutubia watu kwamba kama
serikali 3 zitapita Jeshi litachukua nchi.Hivi ni vitisho ambavyo kwanza
vinampunguzia umakini ama uwezo rais aliyepo madarakani na pia ni
kuamsha hisia za jeshi kufanya hivyo hata leo.Kwa maneno mengine ni
kuwapa mawazo ama maoni wanajeshi wetu kupindua serikali.
Inashangaza sana Mheshimiwa Lukuvi
hawezi kuwajibika kwa kauli hii kwani mwaka 2009 Samson Mwigamba aliwahi
kuandika makala fulani kwenye gazeti la TANZANIA DAIMA kuhusu jeshi
lakini serikali ya ccm ikamfungulia mashtaka mahakamani kwamba ni
mchochezi na analitaka jeshi LIASI TAIFA NA KUFANYA MAPINDUZI ( ARMY
MULTINY AND REVOLUTION) na bahati nzuri sana kesi ile Mwigamba alishinda
mwezi Fenruary 2014.Je serikali haioni kwamba Lukuvi ameamsha hisia na
kufanya uchochezi jeshi kuasi????
Hata hivyo,mimi binafsi nadhani ccm
wanakiinimacho wananchi.Wananchi wamesema Wanataka serikali 3 wao
wanatoa vitosho vya Muungano kuvunjika,wanatoa vitisho kwamba nchi
itaingia vitani,wanatoa vitisho kwamba fanya ufanyalo ni serikali 2 tu
na mwingine akasema kwamba hata kama wananchi wanataka serikali 3 basi
wasubiri yeye aondoke madarakani kwanza.
HIVI statements kama hizo zinaashiria
dalili za nia njema kweli( GOOD POLITICAL WILL) ya kupata katiba mpya
kweli???.Nina mashaka makubwa sana kama kweli katiba mpya inaweza
kupatikana katika hali hii
No comments:
Post a Comment