Tuesday, 22 April 2014

David Moyes atimuliwa Manchester United

Mkufunzi mkuu na meneja wa klabu ya
Manchester United David Moyes ametimuliwa.
David Moyes amefutwa kazi baada ya kushikilia
usukuni wa klabu hiyo kwa miezi kumi tu.
Klabu hiyo hapo awali ilikuwa imekataa
kuzungumzia udaku wa magezti kuwa Moyes
atafutwa kazi kabla ya msimu kumalizika.
Moyes, mwenye umri wa miaka 50, aliteuliwa na
Ferguson kumrithi alipostaafu mwaka jana baada
ya kuwa na klabu hiyo kwa miaka 26.
Taarifa kutoka kwa klabu hiyo imemshukuru
Moyes kwa bidii, uaminifu na hekima
aliyoonyesha kocha huyo akiwa mkufunzi wa
Manchester United.
Moyes alichukuwa usukani wa kuifunza
Manchester United mwaka uliopita baada ya
aliyekuwa kocha wa siku nyingi Sir. Alex
Ferguson kustaafu.
Huku zikiwa zimesalia mechi nne pekee msimu
wa ligi kukamilika Mancheseter united inashikilia
nafasi ya saba kwenye jedwali la msimamo wa
ligi hiyo alama ishirini na tatu nyuma ya viongozi
Liverpool.
Klabu hiyo imeshindwa kufuzu kushiriki michuano
ya ligi ya mabingwa ulaya kwa mara ya kwanza
katika kipindi cha takriban miaka ishirini.

No comments:

Post a Comment