Wiki iliyopita kupitia kipindi cha XXL
na Gazeti la Makorokocho online niliweka hewani ule waraka wa wazi wa
sauti uliosomwa kutoka China na Mwanadada Candy kwa niaba ya Wanadada
wenzake wa Kitanzania walikua wakilalamikia kushikiliwa kama watumwa na
kufanyishwa biashara ya ngono kwa lazima, waraka ule ulikua maalum kwa
wizara ya mambo ya nje na watanzania kwa ujumla kwani kinadada wale
walikua wakiomba msaada warudishiwe Passport zao zilipokonywa na
watanzania wenzao, Binafsi Candy anashikiliwa nchini china tangu
December mwaka jana,
sasa kwa mujibu wa chanzo cha habari cha
kuaminika ni kwamba Candy na Wenzake wamerudishiwa Passport zao ila
simu zao za mkononi wamepokonywa, Candy anawashukuru watanzania wote kwa
kuonyesha kuguswa na kwa vyombo vya habari kwa kuweka hewani waraka
wao, na sasa hivi wako wanatafuta shughuli za kufanya kwani zipo nyingi
sanaaaa China.a
No comments:
Post a Comment