Wednesday, 16 April 2014

KAULI YA AZAM FC JUU YA TUHUMA ZA KUNUNUA UBINGWA WA VPL.

Zikiwa zimepita takribani siku nne tangu Azam
FC ilipoandika historia ya bingwa wa mpya wa
ligi kuu ya Vodacom huku tetesi zikizidi
kuzunguka mitaani kwamba klabu hiyo ya jijini
Dar es Salaam imekuwa ikihonga sana
wachezaji wa timu nyingine pamoja na marefa
ili kujihakikishia ushindi na hatimaye kutwaa
ubingwa kabisa.
“Maneno yanayozungumzwa ni porojo Baada
ya Azam Fc kupata mafanikio ya kuwa bingwa
wa ligi kuu ya Tanzania Bara, Azam Fc ilipata
nafasi ya pili mara Mbili katika Ligi Kuu ya
Tanzania bara haikuwai kusemwa imenunua
leo iweje imekuwa Bingwa isemwe imenunua.
John Bocco ameweka Historia Baada ya
Kufunga Goli la Ushindi ktk Mechi ya Mwisho
ya Ligi Daraja la kwanza na Kuipandisha
Azam Fc kucheza Ligi kuu ya Tanzania Bara,
na leo Hii Tumeshuhudia John Bocco ameweka
Historia ya Kufunga Goli la Ushindi na Kuipa
Timu ya Azam Fc Ubingwa kwa Mara ya
kwanza Tangu ilipopanda Daraja kucheza ligi
kuu ya Tanzania Bara kwa Msimu 2013/2014
na kucheza Bila kupoteza hata mechi Moja.
Hatuto puuzia mechi ya mwisho Dhidi ya JKT
Ruvu Tutacheza kama mechi nyingine
Tulivyocheza Tunahitaji kuweka Historia ya
Kutokupoteza hata Mechi Moja kwa Msimu
Huu JKT Ruvu wajiandae kwa Kichapo wakati
Tukiwa Tunakabidhiwa Kombe letu la Msimu
Huu
Baadhi ya Maneno ambayo Makocha
wanazungumza Sio Mazuri wao kama
wataalam hawatakiwi kujihusisha katika
Propaganda ambazo baadhi ya watu
wanaziendeleza.

No comments:

Post a Comment