Monday, 21 April 2014

BREAKING NEWZZ! MOYES KIBARUA CHAOTA NYASI MAN UNITED

KUNA taarifa zimezagaa kuwa kocha wa
Manchester United, David Moyes
amefukuzwa kazi, japokuwa
haijathibitishwa na familia ya Glazer ambao
ndio wamiliki wa klabu hiyo.
Inasemekana familia ya Glazer imefikia
maamuzi ya kumfukuza kazi bosi huyo wa
Man United ikiwa ni miezi 11 tu tangu
arithi mikoba ya Sir Alex Ferguson.
Msemaji wa Man United amegoma kueleza
kama kweli Moyes amefukuzwa kazi, lakini
imefahamika kuwa kocha huyo hatakuwepo
katika mchezo ujao dhidi ya Nowrich City
kwenye uwanja wa Old Trafford jumamosi .
Kocha mchezaji Ryan Giggs anatarajiwa
kuiongoza Man United mpaka mwishoni
mwa msimu, na wakati huo huo wasaidizi
wa Moyes Steve Round, Phil Neville na
Jimmy Lumsden pia wanatarajiwa
kuondoka na bosi wao.
Kocha wa kudumu wa Mashetani wekundi
anatarajiwa kutangazwa mwishoni mwa
msimu huu.
Familia ya Glazer amechukizwa na kipigo
cha jana cha mabao 2-0 dhidi ya Everton
na kuwa mechi ya 11 kwa Man United
kupoteza katika mashindano yote mwaka
huu.
Moyes alisaini mkataba wa miaka 6 mwezi
mei mwaka jana kurithi mikoba ya Sir
Ferguson aliyestaafu, lakini ameshindwa
kupata mafaniko.
Baada ya familia Glazer kufahamu kuwa
Man United haitamaliza ligi katika nafasi
nne za juu, wameamua kuotesha nyasi
kibarua cha Moyes.
Man United wanaelekea kuwa mabingwa
watetezi waliofanya vibaya zaidi katika
historia ya ligi kuu England kwa kuwa
nafasi ya 7 na kwa mara mwisho Ray
Harford alifanya hivyo na Blackburn Rovers
mwaka 1996. Pia  wanatarajia kukosa hata
ligi ya Europa msimu ujao.
Bodi ya ukurugenzi ya Man United imekuwa
ikimvumilia Moyes kwa matokeo mabaya,
lakini walikerwa sana hasa walipofungwa
nyumbani na wapinzani wao wakubwa
Liverpool na Manchester mwezi uliopita.

No comments:

Post a Comment