WINGA Gareth Bale yuko shakani kuichezaea
Real Madrid katika Nusu Fainali ya Kwanza ya
Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya mabingwa wa
Ujerumani, Bayern Munich kutokana na
kusumbuliwa nugonjwa wa mafua.
Nyota huyo wa Wales hajasafiri na wenzake kwa
ajili ya mchezo wa kwanza leo Uwanja wa
Sangtiago Bernabeu.
Kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti pia
anatilia shaka uzima wa Cristano Ronaldo.
Nyota huyo wa Ureno anatarajiwa kufanyiwa
vipimo vya afya muda mfupi kabla ya mchezo
wa leo.
Shaka tupu: Gareth Bale anasumbuliwa na mafua
kuelekea mchezo wa leo dhidi ya Bayern Munich
Ikiwa Bale ataukosa mchezo wa leo, litakuwa
pigo kwa Ancelotti, ambaye alimwagia sifa nyingi
winga huyo katika Mkutano na Waandishi wa
Habari kuelekea mchezo wa leo.
Bale anang'ara kwa sasa, baada ya kufunga bao
la ushindi katika fainali ya Copa del Rey dhidi ya
Barcelona wiki iliyopita na kocha wake akasema
mchezaji huyo aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 86
kutoka Tottenham atakuwsa mkali zaidi msimu
ujao Hispania ambao utakuwa wa pili kwake
Real.
"Gareth ni mtoto mkali,"alisema Ancelotti.
"Anavutia kwa kujiamini kiasi cha kutosha
hususan kutokana na bao alilofunga dhidi ya
Barcelona katika fainali,"alisema.
No comments:
Post a Comment