Mwanariadha wa Afrika kusini Oscar Pistorius
amerejea tena mahakamani kuhojiwa zaidi na
kujibu maswali ya mwendesha mashtaka mkuu
Gerrie Nel katika kesi anayoshtumiwa kwa
kumpiga risasi na kumuua mpenzi wake
mwanamitindo Reeva Steenkamp nyumbani
kwake mwezi februari tarehe 14 mwaka uliopita .
Bwana Nel amekuwa akimwandama Pistorius ,
akisema hakuwa mkweli katika toba yake na
alimfokea mpenzi wake Reeva Steenkamp mara
kwa mara .
Siku ya kwanza ya maswali ya mahakama dhidi
yake Nel alianza kwa kuonyesha picha za kutisha
za kichwa kilichochuruzika damu cha Bi
Steenkamp, baada ya kupigwa risasi na Pistorius.
Mwanariadha huyo anadai hakumuua makusudi
bali alidhani ni mtu alievamia nyumba yake.
Ameiambia mahakama kuwa alimpenda sana
mwanadada huyo Reeva .
Kiongozi wa mashataka amemsuta Pistorious
akisema kuwa alikuwa ni mbinafsi sana kwa
mpenzi wake na kuwa kile alichokijali sana
ilikuwa ni sifa zake na hadhi yake katika jamii.
Pistorious alikanusha madai hayo akisema
anajuta kwanini hakuwahi kumwambia Reeva
kuwa anampenda kupitia ujumbe wa simu ya
mkononi.
Pistorius akitoa ushahidi
Mwanariadha huyo alikuwa na wakati mgumu
kuelezea mahakama kwanini Reeva alimlaumu
kwa kumuonea katika moja ya ujumbe wa simu
ya mkononi wa WhatsApp ambao alimwandikia
Oscar''tangu turejee kutoka cape town
umekuwa ukinionea sana .''
Viongozi wa mashtaka wana imani kuwa
alimuuwa kimakusudi ndani ya choo chake baada
ya kuzozana.
Mwanariadha huyo mlemavu mwenye umri wa
miaka 27, ambaye hana miguu yake yote mawili,
huenda akahukumiwa jela maisha iwapo
atapatikana na kosa la kuuwa.
Kinyume ya hali ilivyokuwa Siku ya Jumanne,
alipolia kizimbani alipokuwa akielezea yaliyojiri
nyumbani kwake kabla na baada ya mauwaji
hayo,
leo alionekana mjasirii na mtulivu akimjibu
Kiongozi wa mashataka ya umma bwana Nel.
Mamake Reeva bi June Steenkamp amesema
kuwa japo aliombwa msamaha na Oscar moyo
wake haukumsamehe kwani hadi hapo Oscar
hakukiiri alimua bali alisisitiza kuwa anaomba
msamaha kwa kusababisha kifo chake..
Bi Steenkamp mahakamani
Bi Steenkamp alishangaa iwapo Pistoriuos
alikuwa anaigiza au la kwani amekuwa akilia na
kutapika mahakamani .
Katika tukio lingine Oscar alikataa katakata kuwa
alifyatua risasi katika mkahawa mmoja
alipoulizwa na kiongozi wa Mashtaka bwana Nel.
Pistorious alisema kuwa hakujua bunduki hiyo
ilikuwa na risasi.
Iwapo hatapatikana na hatia ya kukusudia kuua
Reeva ,basi kulingana na sheria za Afrika Kusini,
Pistorious huenda akashtakiwa kwa kosa la kuua
bila ya kukusudia ambayo hukumu yake ni kati ya
miaka 6- 15 jela.
Mbali na shtaka la mauaji, Pistorius anakabiliwa
na shtaka la kufyatua bunduki hadharani na
shtaka lingine la kumiliki risasi kinyume na sheria.
Friday, 11 April 2014
PISTORIUS HALI YAZIDI KUA TETE MAHAKAMANI.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment