NI lipi hujasikia? Linaweza kuwa hili! Binti mmoja aliyetambulishwa
kwa jina la Fauzia (jina la mbele lipo), mwenye umri wa miaka 16, mkazi
wa Kigogo jijini Dar amedai kutumikia nafasi ya umalkia katika imani
yenye utata duniani ya Freemason, Uwazi linakudondoshea.
Binti huyo alikwenda mbele zaidi kwa kudai kwamba ili kujiunga na imani hiyo, alimuua mama yake mdogo kwa ajili ya kafara.
Akizungumza na gazeti hili siku chache baada ya kuokoka akiwa
nyumbani kwa baba yake mdogo, Kigogo, Fauzia alisema alitokea Wilaya ya
Kahama mkoani Shinyanga alipokuwa akiishi na bibi yake.
Alikuja Dar kwa lengo la kuendeleza mauaji ya kafara ambapo safari
hii ilikuwa amuue mama yake mdogo mwingine ambaye ni mjamzito kwa sasa.
Alisema kama angefanikiwa kumuua, angepandishwa cheo na kuwa malkia kamili katika jamii hiyo inayotafsiriwa vibaya duniani.
ALIKOTOKEA
Fauzia alisema kuwa mara ya kwanza
hakujua kama amekuwa mwanachama wa Freemason bali alichojua yeye
alijiunga na uchawi wenye ushirika wa Kahama na Kigogo jijini Dar es
Salaam ambapo mara kwa mara alikuwa akija Dar usiku na kufanya mambo ya
kichawi kwa watu mbalimbali.
Alisema siku moja aliambiwa lazima amtoe uhai mama yake mdogo, naye
kwa uwezo aliokuwa nao alifanya hivyo, mama yake mdogo akafa kwa kuugua
ghafla.
Baada ya kifo cha mama yake mdogo, ndipo usiku mmoja bibi kizee mmoja
(alimtaja jina) alimtokea katika ulimwengu wa kiroho na kumwambia
alitakiwa aende kwenye Jiji la Lagos nchini Nigeria kwa ajili ya
kutambulishwa rasmi na kupewa umalkia mdogo.
SAFARI YA NIGERIA ILIVYOKUWA
Akiendelea kuzungumza huku akionekana kujiamini licha ya umri wake mdogo, Fauzia alisema:
“Siku nilipoondoka kwenda Nigeria nilikuwa na wenzangu
walionisindikiza. Ilikuwa ni safari ya kimiujiza. Tulipofika kule, wao
waliniacha mahali, mimi nikajikuta nikitokea ndani ya jengo kubwa ambalo
ndani yake nilikuta mtu mwenye asili ya Kiarabu.
“Yule mtu alinipokea na kuishi naye. Siku moja aliniambia Fauzia wewe una na nguvu mbili, za Freemason na uchawi,” alisema.
ASIMIKWA KUWA MALKIA MDOGO
Aliendelea kusema:
“Ndipo siku moja ikafika, nikasimikwa kuwa malkia mdogo kwa kukabidhiwa
gauni fupi jeupe na kitambaa cheupe cha kuvaa kichwani (vilioneshwa kwa
waandishi wa habari hii).
Hizi nguo ni dalili kwamba anayemiliki ni malkia mdogo. Unakuwa na uwezo wa kujua mambo yote ya siri ya kidunia yanayoendelea.
“Baada ya hapo, nilirejea hapa nchini kwetu. Nilipokewa na bibi
ambaye alikuja kimazingara. Bibi aliniuliza ni wapi nilikokuwa mpaka
nimepata nguvu za Freemason wakati yeye alinikabidhi uchawi wa kawaida?
Sikumjibu,” alisema Fauzia mbele ya baba yake mdogo na mama yake mdogo
aliyekuwa amuue.
AKUMBUKA SIKU YA KWANZA KUJIUNGA NA FREEMASON
Katika mazungumzo hayo yaliyohudhuriwa pia na majirani, binti huyo
akakumbuka jambo zito lililomtokea akiwa darasa la saba na kusema:
“Nakumbuka nikiwa darasa la saba, siku moja usiku niliota ndoto.
Nilimwona mzee mmoja mwenye mapembe akinijia na kunikabidhi mikoba.
Naamini yule mtu ndiyo aliniingiza kwenye Freemason kwani kuanzia pale
ndipo nilipobadilika na kuwa na uwezo wa kuja Dar na kurudi Kahama kwa
usiku moja.
“Basi, baada ya kurudi nyumbani Kahama, siku moja nikaambiwa na
wakubwa wangu natakiwa kwenda nchini Marekani kwa ajili ya kuongeza
nguvu za Freemason.
“Kule nilikaa kwa siku kadhaa na nikafundishwa mambo mengi ya ajabu,
pia nilikutana na viongozi wakubwa wa kidini na kiserikali wa hapa
nchini Tanzania (aliwataja majina).
MAISHA YA NYUMBANI AKIWA SAFARINI
“Ilivyokuwa ni
kwamba, kila nilipokuwa safarini, nyumbani nilikuwa naacha jini
lililofanana na mimi kwa kila kitu. Jini hilo lilifanya kazi nyumbani
badala yangu pasipo mtu yeyote kufahamu wakijua ni mimi. Niliporudi na
jini liliondoka.
ATOBOA SIRI ZA SCREEN TOUCH
“Nikiwa katika jengo la ajabu la Freemason nchini Marekani, niliona
watu wengi wakitengeneza simu za kisasa ‘screen touch’ na televisheni za
‘flat screen’ nilipowauliza za nini? Walinijibu kuwa simu hizo
zimewekwa kifaa maalumu cha kunyonya damu ya mtumiaji kutoka kwenye
kidole chake kila mara atakapobofya.
“Zamani kulikuwa na simu zikitumia peni maalum kwenye screen lakini
Freemason waliamua kuziondoa kwa kuwa hazikuwa zikiwapelekea damu. Hivyo
mtumiaji wa simu za screen touch za sasa lazima aguse kwa kidole chake
na si kwa kitu kingine ndipo ataweza kutumia simu yake ilimradi tu
achangie damu yake kwenye benki za damu za Freemason zilizopo Marekani.”
KUHUSU TV FLAT SCREEN
Akifafanua kuhusu runinga
za flat screen, Fauzia alisema kuwa, hizo zimewekewa kifaa chenye mionzi
ya ki-Freemason ambacho humfanya mtu anayeangalia kila wakati kuwa
zezeta huku vifo vya ghafla akivitaja kama matokeo makuu ya kuangalia
televisheni hizo.
AZUNGUMZIA SURUALI MAARUFU ZA SKIN TIGHT
Mbali na hayo, binti huyo alizizungumzia suruali maarufu za wasichana zinazotambulika kwa jina la ‘skin tight’ ambazo hubana.
Alisema suruali hizo zimewekwa nyuzi maalum za kijini ambazo
husababisha mwanaume yeyote ambaye atamuona msichana akiwa katika vazi
hilo amtamani kingono hata kama msichana huyo havutii.
PASAKA NA X-MASS
Binti huyo alizidi kutia hofu
watu pale aliposema kuwa Sikukuu za Pasaka na X-Mass zimekuwa kubwa
duniani kwa sababu Freemason wametia mkono kwa kuzikuza na kutumbukiza
akilini mwa watu tabia ya dhambi.
“Wengi wanaziona sikukuu hizo ndiyo za kufanyia maasi, kama vile
ngono, ulevi kupitiliza na kufuru nyingine na wanaopotezewa uhai kwa
ajili ya sikukuu hizo ni wengi sana,” alisema.
KUHUSU KUMUUA MAMA YAKE MDOGO
Kuhusu jaribio la
kumuua mama yake mdogo, Fauzia alisema alishindwa mara zote kwa kuwa
alikuwa ‘mzito’. Aliwataarifu Freemason wenzake wamuue lakini nao
walishindwa na kudai kuwa alikuwa akiwaka moto.
Alidai kuwa mama mdogo huyo hakujua lolote lililokuwa likiendelea
mpaka pale alipofika mpwa wao ambaye ni mlokole na kumuombea Fauzia.
MJOMBA MTU AZUNGUMZA
Akizungumza na waandishi
wetu, mjomba wa Fauzia aliyejitambulisha kwa jina la Gervas ambaye ni
mlokole, alisema kuwa kila mara alipokuwa akimuangalia binti huyo,
alihisi ana mambo tofauti na binadamu wengine.
Alisema: “Siku moja nilimsikia roho wa Mungu akiniongoza kufika
nyumbani hapa na kuomba. Nilijikuta nikimuita Fauzia na kuanza
kumuombea.
“Nilishangaa sana kumwona akipandisha mashetani na kuzungumza mambo
ya kutisha aliyodai kuyafanya kwa siri. Baada ya maombi ya muda mrefu
nikisaidiwa na familia yangu ndipo nilipovitoa vifaa vya ajabu.”
BABA MDOGO AZUMGUMZA
Akizungumza na waandishi wetu, baba mdogo wa Fauzia aliyejitambulisha
kwa jina la Amos Deda ambaye anaishi na binti huyo Kigogo na ambaye mke
wake ndiyo alikuwa auawe, alisema:
“Sikuwa nikiamini kabisa
kuhusiana na masuala haya mpaka nilipojionea mwenyewe vifaa hivi vya
kichawi vya Freemason vikitolewa na mjomba wake.
“Fauzia ameniomba msamaha, pia ameomba msamaha kwa familia. Lakini
pia akasema ajali iliyomvunja miguu shangazi yake miaka ya nyuma na
kumuua mtoto wa shangazi yake huyo aliisababisha yeye, pia akaomba
msamaha. Tumeupokea.”
Pia Fauzia aliiomba radhi kwa familia ya mama yake mdogo ambapo
alidai kumuua mama huyo kwa kushirikiana na mkubwa wake mwingine.
NENO LA MWISHO
“Kwa sasa nimeokoka, nimeachana kabisa na mambo haya, zaidi ninamtumikia Mungu kwa nguvu zangu zote,” alisema Fauzia.
No comments:
Post a Comment