Ikiwa leo ndio kumbukumbu ya siku
ya kuzaliwa kwake raisi wa Manzese,
Madee. Tarehe 25 mwezi kama huu,
wasanii mbali mbali wametokea
kumtakia maisha marefu na wengine
kumpongeza kwa njia mbali mbali,
ila kwa hii ya Diamond Platnum ni
kali kuliko yote, Diamond ameamua
kushusha ya kwake yamoyoni kupitia
account yake ya instagram, katika
kukubali juhudi zake, kama msanii
mkongwe na kumshukuru kwa yote.
“Naamini moja ya kitu
kinachokufanya uzidi kufika mbali
na kufanikiwa zaidi ni jinsi ulivyo
na upendo kwa wasanii wote..
hususan upcoming, Nimenza
kukuskia kabla sjui lini nami
ntakuwa flani hadi leo kufikia hapa
lakini skuzote umekuwa ukinisuport
tangu naanza hadi sasa na
kunielekeza katika kazi zangu
mbalimbali… Nakuheshim sana Bro!
Happy birthday.. Mungu akupe
maisha maref yenye amani na
mafanikia tele… Eta Tudele!”
alimalizia Diamond Platnumz
Wednesday, 23 April 2014
HUU NDIO UJUMBE WA DIAMOND PLATNUMZ KWA MADEE...UNA MAANA NZITO SANA...SOMA HAPA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment