Monday, 14 April 2014

KAULI YA MKUU WA MKOA WA ARUSHA JUU YA BOMU LILILOLIPUKA JANA USIKU NA IDADI YA MAJERUHI.

Usiku wa April 13 2014 kwenye baa iitwayo
‘Arusha night park’ iliyopo Mianzini Arusha
ambayo siku zote ni miongoni mwa sehemu
zinazokua na mkusanyiko wa watu wengi
kuanzia jioni, limerushwa bomu wakati watu
mbalimbali wakitazama mpira.
KITOMIXNEWS.. imepata nafasi ya kuongea na
mkuu wa mkoa wa Arusha ambae ni kiongozi
wa Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa
ambae amethibitisha kwamba ni watu 15
wamejeruhiwa kwenye mlipuko huo.
Anasema wote wamepelekwa hospitali ambapo
uchunguzi wa awali umeonyesha bomu hilo ni
la kutengenezwa kwa mkono na mpaka sasa
hajajulikana alietekeleza shambulio hilo.
Kwenye sentensi nyingine pia amesema hakuna
aliepoteza maisha kwenye shambulio hilo
ambalo uchunguzi wa awali umeshatoka, ila
baadae itatoka taarifa rasmi pale uchunguzi
kamili utakapokamilika.

No comments:

Post a Comment