Ni visa mbavyo wengi tulivisikia katika hadithi
za kale, watu kuliwa na majitu, lakini katika
siku za karibuni tumeshuhudia watu wakila
viungo vya wenzao Jamhuri ya Afrika ya Kati
katika jazba ya kulipiza kisasi dhidi ya watu
waliowadhulumu katika uongozi uliong'olewa
mamlakani wa Seleka .
Nchini Pakistan Polisi wamewakamata wanaume
wawili kwa makosa ya kuiba maiti ya mtoto
kutoka kaburini na kisha kumla.
Wawili hao Arif Ali na kakake Mohammed Farman
Ali waliachiwa huru baada ya kuwa jela kwa
miaka miwili kwa kula nyama ya binadamu.
Hata hivyo wawili hao wameonekana kuwa na
tamaa kubwa ya mchuzi wa nyama ya
binadamu.Wakaazi hao wa kijiji cha Daryabn
Khan jimbo la Punjab walikamatwa mwaka 2011.
Polisi walisema kwamba walipata kiwiliwili cha
maiti ya msichana mdogo kikiwa bila miguu na
mikono.Wawili hao walikiri kwamba walipika
mchuzi wa nyama ya viungo hivyo na kuvila.
Walishtakiwa kwa makosa ya kuharibu kaburi
kwani nchini Pakistan hakuna sheria
inayozungumzia hatia ya mtu kumla mwenzie.
Punde baada ya kuachiwa Arif Ali aliambia BBC
kwamba anajutia makosa hayo na kwamba
hatarudia tena.
Hata hivyo punde si punde polisi wamesema
waliitwa na majirani wa jamaa huyo
wakilalamikia uvundo mkali kutoka kwa nyumba
yake.
Walipoingia chumbani humo Lo ! wakapata
kichwa cha mtoto.Kiwiliwili hakijulikani kililiwa au
kapotelea wapi. Arif Ali tena amekamatwa kwa
mara ya pili na polisi wanaendelea kumsaka
kakake.
Polisi wanaamini ndugu hawa walifukua maiti ya
mtoto ambaye kichwa kilipatikana ndani ya
makaazi yao.
Arif anamlaumu kakake Farman.Wawili hao
waliwahi kuoa na hata wakajaliwa watoto, hata
hivyo wake zao waliwatoroka kabla ya
kukamatwa kwao na kufungwa jela kwa kisa cha
awali.
Tuesday, 15 April 2014
MTU MMOJA AKAMATWA AKILA MAITI YA MTOTO HUKO PAKISTANI..
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment