Friday, 11 April 2014

KUHUSU HABARI ZA MSANII SHETTA KUPATA AJALI YA GARI

Msanii Shetta wa bongofleva amepata ajali ya
gari maeneo ya Minjingu akielekea Babati kwa
ajili ya kufanya show ambayo maamuzi ya
kuifanya yalikuja dakika za mwisho.
Wakiwahi show kwa kutumia usafiri wa gari aina
ya Noah, walipata hiyo ajali jioni ya April 11
2014 baada ya gari kupinduka wakati dereva
akiwa kwenye jitihada za kumkwepa Punda.
Kwenye gari hilo, Shetta alikua na Msaidizi wake
pamoja na Waandaaji wa show ambapo hakuna
aliepoteza maisha isipokua majeraha
madogomadogo huku yeye mwenyewe akiumia
kichwani na mguuni.
Shetta alipelekwa hospitali lakini baadae
aliruhusiwa kuondoka na kuendelea na safari
japo haijajulikana kama aliweza kufanya hiyo
show baada ya kugundua kwamba alikua
ameumia kidogo.

No comments:

Post a Comment