Wednesday, 16 April 2014

ALICHOKISEMA WAKALA WA MCHEZAJI TONI KROOS KUHUSU KUHAMIA MAN UNITED.

Tetesi za usajili wa mchezaji wa FC Bayern
Munich Toni Kroos zimezidi kutengeneza
vichwa vya habari katika media.
Wakati mapema wiki hii kocha wa Bayern Pep
Guardiola akisema kwamba hatma ya mchezaji
ipo mikononi mwake mwenyewe, leo hii wakala
wake amezungumza na kauli inayoonyesha
mchezaji huyo anaweza kubaki Bayern Munich
mpaka mkataba wake utakapoisha mnamo
2015.
Muda mfupi baada ya Guardiola kusema
kwamba hatma ya mchezaji ipo mikononi
mwake mwenyewe, gazeti la Guardian la
Uingereza likaripoti kwamba Manchester United
imempa ofa ya mshahara wa paundi 260,000
kwa wiki, fedha ambayo itakuwa ni mara nne
ya anayopata sasa 72,000 pounds kwa wiki.
Lakini leo Jumatano wakala wa mchezaji
huyo Volker Struth, amesema United
haijawafuata rasmi kuhusu suala la kutaka
huduma za mchezaji huyo.
Alisema: “Hakuna ofa rasmi ya mkataba na
Bayern. Pia zaidi sidhani kama kuna hitaji la
kutoa ofa mpya, kwa sababu Toni Kroos
ataendelea kuichezea Bayern mpaka 2015.”
Wakala huyo ameshaonekana akiwa pamoja na
kocha United David Moyes takribani mara mbili
katika miezi ya hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment