Monday, 21 April 2014

WAANDISHI WA HABARI WAISHI MIEZI 6 GIZANI NA MIEZI 2 NA NUSU WAKIWA WAMEFUNGWA MINYORORO BAADA YA KUTEKWA..

Wanahabari wanne wa Ufaransa walioachiliwa
baada ya kutekwa nyara na wanamgambo nchini
Syria karibia mwaka mmoja uliopita wamewasili
nchini Ufaransa.
Waandishi hao wamekuwa wakisimulia masaibu
yao walipokuwa mikononi mwa watekaji wao
wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa kiisilamu
wenye uhusiano na kundi la Al Qaeeda.
Mmoja wa waandishi hao, Didier Francois,
alisema kuwa walifungwa kwa minyororo kwa
pamoja na kufungiwa katika chumba kisicho na
mwangaza
Mwenzake Nicolas Henin, alisema kuwa watekaji
wao hawakuwatendea vizuri.
Bwana Henin na Francois wakiandamana na
Edouard Elias na Pierre Torres, waliamkuliwa na
familia zao pamoja na Rais Francois Hollande
walipowasili nchini Ufaransa.
Kuokolewa
Walipatwa na wanajeshi wa Uturuki wakiwa
katika mpaka wa Syria na Uturuki
Kundi la wapiganaji la 'Islamic State of Iraq' lenye
uhusiano na kundi la Al Qaeeda limetuhumiwa
kwa utekaji huo.
Picha za wanaume hao ziliwaonyesha wakiwa
wamechakaa ingawa walikuwa bukheri wa afya.
Bwana Francois,mwenye umri wa miaka 53,
alisema alikuwa na furaha sana kwani yuko huru,
ameweza kuona mbingu, kutembea na
kuzungumza bila kikwazo chochote.
"tuliishi kwa miezi sita gizani huku miezi miwili
na nusu tukiwa tumefungwa kwa minyororo,''
aliambia kituo kimoja cha redio anachokimiliki.
"tuliona siku ndefu , ingawa hawakuwahi
kupoteza matumaini,'' aliongeza bwana Francois.
Waandishi hao walipatikana wakiwa
wamefunikwa nyuso zao na kufungwa minyororo
katika sehemu moja ya mpakani mwa Syria na
Uturuki.
Waliokolewa na wanajeshi wa Uturuki.
Wanaume hao walitoweka katika matukio mawili
tofauti mwezi Juni mwaka jana.
Bwana Francois, ni mwandishi mwenye uzoefu wa
miaka mingi na Elias ni mpiga picha. Wote
walitekwa nyara wakielekea mjini Aleppo.
Henin, alikuwa anafanya kazi na jarida la Le Point
huku bwana Torres, akiripotia kituo cha
televisheni cha channel Arte, walitekwa nyara
baadaye mwezi huo karibu na eneo la Raqqa.
Zaidi ya waandishi 60 wameuawa nchini Syria
tangia kuanza kwa mgogoro dhidi ya serikali ya
rais Bashar al Asaad miaka mitatu iliopita.

No comments:

Post a Comment