Sunday, 13 April 2014

BARCELONA YAPIGWA NA KITIMU HICHO HADI AIBU

KLABU ya Barcelona imetimisha wiki ya
machungu baada ya kufungwa bao 1-0 na
Granada katika La Liga na kujiweka katika
mazingira magumu ya kutetea ubingwa, siku
chache baada ya kutolewa katika Ligi ya
Mabingwa Ulaya.
Bao la mapema la Yacine Brahimi lilitosha
kuwalizaa tena mabingwa wa zamani waq Ulaya
na sifa zimuendee kipa Orestis Karnezis,
aliyezuia michomo mingi akiichezea kwa mara
ya pili klabu hiyo, akiwatoa kapa Lionel Messi na
wenzake.
Barcelona inabaki na pointi zake 78 baada ya
mechi 33 katika nafasi ya pili, nyuma ya vinara
Atletico Madrid na wababe wao waliowatoa
Ulaya, wenye pointi 79 za mechi 32, wakati Real
Madrid ina pointi 76 za mechi 32 pia.

No comments:

Post a Comment