Sunday, 13 April 2014

ARSENAL YATINGA FAINALI KOMBE LA FA

ARSENAL imetinga Nusu Fainali ya Kombe la FA
baada ya kuitoa Wigan kwa penalti 4-2 kufuatia
sare ya 1-1 ndani ya dakika 120 Uwanja wa
Wembley usiku huu.Baada ya kuitoa timu hiyo ya
Ligi Daraja la Kwanza England,maarufu kama
Championship, Arsenal sasa itakutana ama na
Hull City au Sheffield United Mei 17 katika fainali
Uwanja huo huo wa Wembley.
Ikiwa haijashinda taji lolote tangu waliposhinda
Kombe la FA mwaka 2005, Arsenal ilionekana
kupania kufanya vizuri leo, ingawa iliuanza
mchezo vibaya.
Wigan ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya
63 kupitia kwa Jordi Gomez aliyefunga kwa
penalty baada ya beki wa Arsenal, Per
Mertesacker kumuangusha kwenye eneo la hatari
Callum McManaman.
Hata hivyo, beki huyo Mjerumani ndiye aliyeifufua
Gunners katika mchezo wa leo baada ya kufunga
bao la kusawazisha dakika ya 82 na mchezo
ukahamia kwenye muda wa nyongeza.
Penalti mbili za mwanzo za Wigan ziliokolewa na
kipa Lukasz Fabianski, kabla ya kiungo wa
Arsenal, Santi Cazorla kufunga penalti ua ushindi
na kuipeleka timu hiyo fainali.

No comments:

Post a Comment