Toka March 8 2014 mpaka leo ikiwa ni
May, ndege ya Malaysia iliyokua imebeba zaidi ya watu 200 haijulikani
ilipo baada ya kupotea ikiwa inatokea Malaysia kwenda Beijing China.
Kwa siku zote hizo toka imepotea ndugu
wa abiria wa ndege hiyo wamekua wakishinda kwenye hoteli ambazo pia
zimekua zikitumiwa na shirika hilo la Malaysia kukusanyika na kutoa
taarifa kuhusu kinachoendelea kwenye kuitafuta ndege hiyo.
May 1 2014 taarifa zimeanza kusambaa
kwamba ndugu hao sasa wamepewa maagizo waondoke kutoka kwenye hoteli
zote walizofikia Beijing na Kuala Lumpar na kurudi nyumbani kwao ambapo
taarifa za chochote kitakachotokea watazipata wakiwa hukohuko majumbani.
Hii iliwafanya ndugu kadhaa kuangua tena
vilio na kupiga mayowe baada ya kujua kwamba taarifa ya shirika hilo la
ndege inamaanisha haitakuwepo tena ile mikusanyiko ya kila siku kwenye
chumba cha mikutano kwa ndugu hao kupewa taarifa za kinachoendelea
kwenye zoezi la utafutaji wa ndege hiyo.
Kwenye hoteli ya Lido Beijing ambako
kampuni hiyo ya ndege imekua ikiwalipia ndugu hao wa abiria toka ndege
ipotee, kulikua na watu wanaozidi 500 ambao wote ni ndugu wa abiria
waliopotea.
Hata hivyo kampuni hii ya ndege itaanza
kutoa malipo ya pesa kwa ndugu hao siku za karibuni ambapo japo
haijasema itatoa kiasi gani, sheria inasema ndugu wanaweza kulipwa
kuanzia dola za kimarekani laki moja na nusu mpaka laki moja na elfu 75.
Ripoti mpya iliyotoka inasema maafisa
hawakua wamegundua kupotea kwa ndege hiyo mpaka dakika 17 baadae na
walichelewa kwa dakika 240 kuanza kuitafuta ndege hiyo baada ya kupotea
kwenye radar
No comments:
Post a Comment