WAKATI staa wa muvi za Kibongo, Adam Kuambiana akizikwa jana jijini Dar
es Salaam, msanii mwenzake Aunt Ezekiel amekumbuka kipigo
alichoangushiwa na Kuambiana yeye na Wema, wiki chache zilizopita.Akiteta na kona hii, jana jijini Dar, Aunt alisema: “Nakumbuka hiyo
siku, tulikuwa location, Mikocheni mimi, Wema, Martin Kadinda na wasanii
wengine tukirekodi filamu ya Wema. Kuna kitu tulikosea, Kuambiana
akatupiga mimi na Wema.
“Alikuwa makini sana na kazi yake, hakupenda mzaha unapofika muda wa
kazi. Nikikumbuka ile siku huwa namkumbuka sana Kuambiana kwa kweli.
Mungu ampumzishe kwa amani.”
No comments:
Post a Comment