MSHAMBULIAJI
Samuel Eto'o ameripotiwa kukana madai kwamba yupo karibu kustaafu baada
ya kumuita kocha wake, Jose Mourinho ni 'mpumbavu' kwa kuhoji umri
wake.
Mwanasoka
huyo mwenye umri wa miaka 33 ilivumishwa amekorofishana na Mourinho
baada ya kocha huyo wa Chelsea kuchukuliwa na Televisheni ya Ufaransa
akisema; "Eto’o ana miaka 32, labda 35, nani anajua?".
Pamoja
na hayo Eto'o alionyesha kuchekeshwa na maelezo hayo na kuigiza
kushangilia kama kikongwe akitumia mkongojo baada ya kufunga boa dhidi
ya Manchester United Januari, yakiwa ni majibu kwa kocha huyo Mreno.
Majibu tosha: Samuel Eto'o alifanya hive kushangilia kama kikongwe akipeleka majibu kwa Jose Mourinho aliyehoji umri wake
Akizungumza
na Waandishi wa Habari baada ya kutua Abidjan kwa ajili ya michuano ya
vijana ya Copa Coca Cola michuano inayofanyika mjini Bouake, Eto'o
alisema: "Nina umri wa miaka 33. Na si kwa sababu mpumbavu ameniita mzee
basi unatakiwa kuamini. "Na unatakiwa kujua kwamba, mzee alikuwa bora kuliko nyota chipukizi,".
Eto'o, sass
amemaliza Mkataba wake baada ya msimu huu The Blues, pia amesema kwamba
ni bora angeendelea kucheza klabu ya Ulaya kuliko kwendea Mashariki ya
kati kwa mkataba mnono.
"Baadhi
wanaamini nitakwenda kustaafu Marekani au Mashariki ya Kati, lakini
nimerudiaa furaha ya kucheza Ligi ya Mabingwa na nitaendelea kucheza
Ligi ya Mabingwa,".
![In doubt: Chelsea boss Mourinho was filmed questioning Eto'o's age](http://i.dailymail.co.uk/i/pix/2014/05/15/article-2629112-07C4BE0100000514-843_634x416.jpg)
Ana shaka: Kocha wa Chelsea, Mourinho alikaririwa akihoji umri wa Eto'o
"Wapi?
Sitakuambia. Lakini nitaendelea kucheza, kwa sababu kiakili na kimwili
bado niko vizuri. Hivyo, ninakwenda kwenye Kombe hili la Dunia na
lingine pia wakati nitakapokuwa na umri wa miaka 37. Wengine wamefanya hivi wakiwa na umri wa miaka 42, hivyo ninaweza kucheza kwenye fainali mbili zaidi za Kombe lka Dunia,"alisema.
![Veteran: Eto'o will take part in his fourth World Cup with Cameroon in Brazil this summer](http://i.dailymail.co.uk/i/pix/2014/05/15/article-2629112-09F9A7DC000005DC-193_634x415.jpg)
Mkongwe: Eto'o atacheza fainali za Nne za Kombe la Dunia mwaka huu nchini Brazil
No comments:
Post a Comment