HATIMAYE
`deal done!`. Klabu ya Manchester United amemteua Louis van Gaal kuwa
kocha mkuu mpya kwa mkataba wa miaka mitatu kufuatia kufukuzwa kazi kwa
David Moyes mwezi uliopita.
Mholanzi huyo amechukua nafasi ya aliyekuwa kocha wa muda wa Man United, Ryan Giggs aliyeteuliwa kuwa kocha msaidizi.
Frans
Hoek na Marcel Bout wajajiunga na Van Gaal kama makocha wasaidizi na
mholanzi huyo anakuwa kocha wa kwanza kutoka nje kuiongoza Man United.
Van
Gaal ataanza kazi rasmi baada ya kumalizika kwa fainali za kombe la
dunia mwaka huu nchini Brazil ambako anaiongoza Uholanzi akiwa kocha
mkuu.
Kwanza Va Gaal anatarajiwa kuiongoza Uholanzi kombe la dunia kabla ya kujiunga na Man United
![Values: Van Gaal has a record of bringing through young talent at Ajax, Barcelona and Bayern Munich](http://i.dailymail.co.uk/i/pix/2014/05/07/article-2622185-06616B6F00000514-808_634x448.jpg)
Van
Gaal akiwa na furaha amesema: ‘Siku zote nilikuwa natamani kufanya kazi
ligi kuu ya England. Kuwa kocha Manchester United, klabu kubwa duniani,
inanifanya nijivune”.
“Niliwahi
kucheza mechi Od Traffford kabla na najua namna uwanja huu ulivyo na
hamasa. Mashabiki wanapenda mno mpira. Klabu ina maono ya mbali; nami
pia nina maono makubwa. Kwa pamoja nadhani tutaweka historia.”.
Ryan
Giggs alisema: “Nimefurahi kupata fursa ya kuwa kocha msaidizi. Van
Gaal ni kocha bora duniani na najua nitajifunza vitu vingi kutoka kwake
na kuchangia kadri niwezavyo”.
“Manchester United ni sehemu ya maisha yangu kwa muda mrefu na nimefurahi kuendelea kuwepo na kufanya kazi muhimu kama hii”.
Sehemu
ya taarifa ya Manchester United inasomeka: “Louis van Gaal ataanza kazi
ya ukocha mkuu wa Manchester United kuanzia msimu wa 2014/2015.
Amesaini mkataba wa miaka mitatu”.
No comments:
Post a Comment