From London With Love ...!!! Star mkubwa wa filamu nchini Tanzania
Wastara Juma ambaye kwasasa yupo London Uingereza amevishwa pete ya
uchumba huko na mwanaume anayeonekana hapo pichani. Wastara aliweka
picha kadhaa kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii na wengine
kudhani ni filamu mpya. Star mwenzake pia Riyama Ally ambaye wapo wote
huko London nae aliandika "Ama kweli Mungu akitaka kukupa haandiki
barua......, kila la kheri mama huu mwanzo mzuri kwako". Baada ya kuona
picha hizo haraka sana Swahiliworldplanet ilimuendea hewani Wastara
akiwa huko huko London na kumuuliza kama ni movie au ni kweli, tofauti
na siku zote ambapo kama ni movie Star huyo huweka kweupe lakini safari
hii alionekana hana la kusema pengine kwa furaha na kuishia kujibu kwa
ufupi kwa kusema "No comment" alipododoswa tena alijibu hivyo hivyo tena
"No comment".
Wastara Monalisa, Riyama Ally na Cloud ni takribani wiki tatu sasa wapo
London kwa mwaliko maalum na kucheza filamu inayoitwa Ughaibuni(Abroad)
ambapo tayari wameanza kuishuti. Tungependa kuwatakia kila la kheri
wawili hao .Angalia picha zaidi Wastara akivishwa pete hiyo.
No comments:
Post a Comment