Saturday, 17 May 2014

MATAJIRI WA CONGO, TP MAZEMBE WACHARAZWA 1-0 NA EL HILAL YA SUDAN.

12juillet2012-division1-j9-mazembe-vs-muungano-14_1342119829Na Baraka Mpenja MIAMBA ya soka nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, TP Mazembe imepigwa kidude kimoja kwa yai dhidi ya El Hilal Omdurani ya Sudan katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa barani Afrika.

El Hilal walianza kutibua mipango ya Mazembe katika dakika ya 51 baada ya Salah Al Jizoli kuandika bao la kuongoza kufuatia kumalizia pasi nzuri ya Bakri Babeker.
Kipigo hicho cha bao 1-0 kimewafanya Mazembe kuanza vibaya michuano hiyo na sasa watahitaji kufanya vizuri mchezoz unaofuata, huku wakiwa katika kundi A pamoja na wapinzani wao wakubwa AS Vita. Washambuliaji wote wawili wa Tanzania wa TPM walicheza, Mbwana Samatta akianza na Thomas Ulimwengu akitokea benchi dakika ya 66 kwenda kuchukua nafasi ya Rainford Kalaba.
Samatta na Ulimwengu wanatarajiwa kuondoka asubuhi kuja Dar es Salaam kujiunga na timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kwa ajili ya mchezo wa Jumapili dhidi ya Zimbabwe, kuwania hatua ya makundi ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika mwakani nchini Morocc
RATIBA YA MECHI ZA KESHO NA KESHOKUTWA HII HAPA
 Saturday 17 May 2014
Esperance (Tunisia) v ES Setif (Algeria)   20:00  
Sunday 18 May 2014
AS Vita (Congo DR) v Zamalek (Egypt)   15:30  
CS Sfaxien (Tunisia) v Al Ahly Benghazi (Libya)   18:00  
Saturday 24 May 2014
Al Ahly Benghazi (Libya) v Esperance (Tunisia)   18:00  
Zamalek (Egypt) v Al Hilal (Sudan)   19:30  
Sunday 25 May 2014
TP Mazembe (Congo DR) v AS Vita (Congo DR)   15:00  
ES Setif (Algeria) v CS Sfaxien (Tunisia)   19:30

No comments:

Post a Comment