Suarez amefumania nyavu mara 31
na kutoa pasi 12 za mabao katika mechi 33 za Ligi Kuu alizocheza, huku
timu yake ya Liverpool ikizidiwa na Manchester City kwenye mbio za
ubingwa.
Suarez, ambaye pia ameshinda tuzo ya mchezaji Bora wa Wachezaji
wa PFA na Mchezaji Bora wa Waandishi wa habari za Soka msimu huu,
alinyakua tuzo ya nne msimu huh baada ya Kiatu cha Dhahabu cha Ligi.
Mpachika mabao huyo wa Uruguay,
ambaye anajiandaa kukutana na England katika Fainali za Kombe la Dunia
Juni 19, alimaliza msimu akiwa mfungaji bora- akimzidi kwa mabao 10
mchezaji mwenzake wa Wekundu hao, Daniel Sturridge.
No comments:
Post a Comment