UCHAGUZI
mkuu wa klabu ya Simba umepamba moto kufuatia wagombea mbalimbali
kurejesha fomu kwa mbwembwe akiwemo Michael Wambura anawania nafasi ya
Rais.
Wambura
ambaye ni katibu mkuu wa zamani wa shirikisho la soka Tanzania (TFF)
zamani (FAT) amerudisha fomu hizo akisindikizwa na wanachama mbalimbali
akiwemo kocha wa zamani wa timu hiyo Jamhuri Kihwelo ‘Julio’.
![]() |
Goffrey Nyange 'Kaburu' naye amerejesha fomu leo |
![]() |
Mehdi Burhan Mlanzi naye amerejesha fomu leo |
![]() |
Wambura kulia akikabidhi fomu leo kwa Katibu wa Kamati ya Uchaguzi, Khalid Kamguna |
Licha
ya kuingia kwa mbwembwe na kuteka makao makuu ya klabu hiyo
aliwasilisha fomu hizo kwa dua kali iliyosomwa na Abdurahman Ahmed, na
Godlove Kivate.
Licha ya dua hiyo, Wambura aliihusia kamati ya uchaguzi itoe nafasi kwa wanachama wa klabu hiyo kuchagua viongozi wanaowataka.
“Wanachama
wasikilize sera, uongozi ni dhamani hivyo kamati ya uchaguzi nayo iwape
nafasi watu wachague viongozi wanaowataka,”alisema Wambura.
Wakati
Wambura akiyasema hayo, Julio alitoa kali ya mwaka baada ya kusema
anaidai million 24 viongozi wanaomaliza muda wake wake chini ya
Mwenyekiti wake Ismail Aden Rage.
“Mimi
bado ni kocha wa Simba kwa kuwa uongozi uliompindua Rage kikao chake
kilikuwa sio haliali na mimi bado ni kocha halali wa timu hiyo.
Akizungumza
na BIN ZUBEIRY, Katibu msaidizi wa kamati ya Uchaguzi, Khalidi Kamguna
alisema wagombea 41 wamechukua fomu kuwania uongozi wa timu hiyo.
Alisema
kuwa zoezi hilo limefugwa jana ambapo kwa sasa watapitia fomu hizo
zitapitiwa Mei 17 ambapo Mei 19 wagombea watatangazwa.
Aliwataja wagombea waliochukua fomu kwenye nafasi ya Rais ni Evans Aveva, Michael Wambura, na Andrew Tupa.
Makamu
wa Rais waliochukua ni Geoffrey Nyange ‘Kaburu’, Joseph Itang’are,
Swedi Nkwabi, Bundara Kabulwa, Willbar Mayage na Julio.
![]() |
Jasmine Badawi naye amerejesha fomu |
![]() |
George Wakuganda naye amerejesha fomu |
![]() |
Asha Muhaji naye amerejesha fomu |
Wajumbe
ni Abdulhamid Mshangama, Alfred Martin, Ally Sulu, Iddy.noor Kajuna,
George Wakuganda, Said Tuli, Ramson Athuman, Seleiman Abdul, Khamis
Mkom, Said Pamba, Rodney Chiduo.
Wengine
ni, Collin Frisal, Chano Karaha, Emanuel Kazimoto, Juma Pinto, Salim
Jazaa, Yassin Said, Hussein Simba, Damian Manembe, Ally Chaurembo,
Ibrahim Masoud, Ahmed Mlanzi, Iddi Nassoro, Kessy Kikoti, Maulid Said,
Juma Mussa, Omary Said, Said Kubenea.
Kamguna aliendelea kusema wanawake watatu wamejitokeza ni Asha kigundula, Asha Muhaji, Jasmin Badar na Amina Hussein.
No comments:
Post a Comment