REAL Madrid ya Hispania itafanya ziara Tanzania na lini watakuja itajulikana
kesho katika Mkutano maalum na Waandishi wa Habari wa kutaja rasmi ziara ya
klabu hiyo.
Kampuni ya 1Plus Communications ya Dar es
Salaam chini ya Mkurugenzi wake, Fina Mango
ndiyo waratibu wa ziara hiyo, ambayo hata hivyo itahusisha wachezaji waliowika
kwenye klabu hiyo miaka ya nyuma.
Maana yake tutarajie kuwapokea watu kama Ronaldo Lima, Luis Figo, Zinadine
Zidane, David Beckham, Roberto Carlos na wengineo.
Magwiji hao wa Real wamekuwa wakifanya ziara za mechi za kirafiki nchi mbalimbali duniani na sasa Tanzania inapata bahati ya kuwapokea nyota wa dunia.
No comments:
Post a Comment