Katika hali ya kawaida kufanya mapenzi kuna
faida nyingi, lakini linapokuja suala la kuzidi kiasi
tunapata matatizo ya msingi ambayo huleta
madhara kwa watu wanaoendekeza sana ngono.
Kuna watu ambao hawezi kulala bila kufanya
mapenzi na huku wengine wakikosa uwezo wa
kuvumilia hata kwa siku mbili au tatu.
Mtu anaweza kuwa na mke na kujikuta kila siku
anatumia ‘chakula cha usiku’ kwa sababu tu
hakuna wa kumkataza na kwamba ana haki ya
kufanya hivyo kwa sababu amelipa mahari.
Hilo linaweza kuwa jambo jema kwa upande
mwingine, lakini uchunguzi unaonyesha kuwa
watu wengi kati ya watu wanaolalamika kupoteza
hisia za kimapenzi hutoka katika kundi la watu
wapenda ngono.
Pamoja na tatizo hilo, yapo madhara mengine
mengi ambayo mtu asiyekuwa na kiasi katika
tendo la ndoa anaweza kukabiliana nayo, hivyo ni
vema tukajifunza ili tusiwe watu wa kuendekeza
miili kiasi cha kulazimika kufanya mapenzi kila
tunapokutana hata kwenye nguzo ya umeme na
chini ya miti kwa vile tu miili imetaka kufurahika.
Twende pamoja katika kutazama madhara hayo
kwa kina.
KUPOTEZA HAMU YA TENDO.
Watu wenye pupa za kufanya mapenzi hupoteza
haraka hisia za kimapenzi kwa wapenzi wao
kutokana na sababu za kisaikolojia zinazoweza
kujitokeza wakati wa ufanyaji wa tendo la ndoa
mara kwa mara.
Sababu hizo zinaweza kuwa ni pamoja na zile za
kumzoea mwenza kiasi cha kukosa msisimko
hata anapomuona akiwa mtupu.
Aidha kukinai haraka staili za kimapenzi
kunatajwa kujitokeza kutokana na kukutana mara
kwa mara kwa aina zile zile za mapenzi na
pengine sehemu moja, kitanda kimoja na chumba
kile kile, jambo ambalo linaweza kumfanya
mhusika asione jipya kutoka kwa mwenza wake
na hivyo kupoteza hamu naye na kuhisi kama
hawezi tena kushiriki tendo la ndoa kikamilifu.
KUUJAZA MWILI TAMAA KUBWA.
Tabia ya kufanya mapenzi mara kwa mara
huongeza uzalishaji wa homoni mwilini na
kuufanya mwili uwe na msukumo mkubwa wa
kutaka kuridhishwa kwa tendo la ndoa bila
kukosa na hivyo kumfanya mhusika asiwe mtu
mwenye uwezo wa kuzuia tamaa na kukosa
chaguo la nani wa kufanya naye mapenzi na kwa
wakati gani?
Watu wanaojiendekeza katika kufanya mapenzi
mara kwa mara ndiyo wale ambao kila
wanayemtazama barabarani humtamani bila kujali
hadhi yake.
Hawa ndiyo wanaobaka, kusaliti ndoa zao hata
kwa watumishi wa ndani au kufanya mapenzi na
watoto wao wa kuwazaa kwa vile akili zao huwa
zimeathirika kwa tamaa ya mapenzi.
Unapokuwa mtu wa kufanya mapenzi mara kwa
mara huwezi kuwa na uwezo wa kuzuia tamaa
yako. Mumeo akiondoka siku mbili unatamani
kuwa hata na houseboy ili akukate kiu ya penzi.
KUPOTEZA RAHA KAMILI YA TENDO.
Raha ya tendo hutegemea sana hisia iliyokuzwa
kutokana na mapenzi sahihi na kiu ya kufanya
mapenzi, hivyo basi ukiwa mtu wa kufanya
mapenzi kila mara unaweza kupoteza msisimko
wa tendo na kujikuta unapata furaha ambayo
haikutoshi kumaliza tamaa yako.
Kama ni mapenzi utakuwa unayafanya kwa
mazoea tu na msisimko wako utakuwa mdogo!
KUPOTEZA NGUVU ZA MWILI.
Madhara mengine yanayoweza kupatikana kwa
kufanya mapenzi mara kwa mara ni pamoja na
kupoteza nguvu nyingi za mwili.
Kama tujuavyo tendo la ndoa hasa kwa wanaume
huwafanya watumie nguvu nyingi, hivyo kuufanya
mwili uchoke. Aidha lishe inapokuwa ndogo kwa
wafanya mapenzi mwili hukosa nguvu za kutosha
kuhimili misukosuko ya kimaisha.
Sambamba na hilo mbegu za uzazi zinazotoka
kwa wanaume wanaofanya mapenzi mara kwa
mara huwa dhaifu.
KUPATA MAGONJWA.
Kama tulivyojifunza kuwa watu wanaofanya
mapenzi mara kwa mara huwa na tamaa na
hujikuta wanafanya mapenzi holela ambayo
huweza kuwasababishia magonjwa ya zinaa
ukiwemo ukimwi, lakini ufanyaji wa mapenzi
usiokuwa na msukumo wa kutosha hasa kwa
wanawake huwafanya waishiwe msisimko na
kuzifanya sehemu zao za siri kutotoa ute
unaoweza kuwakinga na michubuko wakati wa
kujamiiana na hivyo kuwasababishia michubuko
itakayoweza kuleta maambukizi ya haraka ya
magonjwa ya zinaa ukiwemo
Wednesday, 21 May 2014
HAYA NDIO MADHARA YA KUFANYA MAPENZI KUPITA KIASI...!! SOMA HAPA KUFAHAMU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment