Tuesday, 20 May 2014

HAWA NDIO WACHEZAJI WANATARAJIWA KUSAJILIWA NA MAN U..MSHAHARA WA VAN GAAL NA ATAPEWA PAUNI MIL 200 KUSAJILI


Winged wonder: Bayern Munich star Arjen Robben is being considered by his national manager as a targetKOCHA Louis van Gaal atakuwa analipwa mshahara wa Pauni Milioni 6 kwa mwaka na atapewa Pauni Milioni 200 kwa ajili ya kufanya usajili wa maana Manchester United.
Kocha huyo Mholanzi aliyeteuliwa kuchukua nafasi ya David Moyes, amesaini Mkataba wa miaka mitatu na kutangazwa rasmi mchana wa jana na atakuwa anasaidiwa na Ryan Giggs.
Klabu bado inataka kujumuisha watu watatu wa Class of 92 katika bench la Ufundi, Phil Neville, Nicky Butt na Paul Scholes -lakini bado hakuna uamuzi uliotolewa hadj sasa.
Van Gaal ataanza kazi rasmi baada ya Fainali za Kombe la Dunia mwezi ujao nchini Brazil ambako ataiongoza Uholanzi kwa mara ya mwisho.
Van Gaal anataka kuwasajili mabeki Wajerumani Mats Hummels na Holger Badstuber, viungo Toni Kroos na Arjen Robben na mshambuliaji Mario Mandzukic kuimarisha Man United ya kushindani mataji msimu ujao.
Kocha mpya: Louis van Gaal atapewa Pauni Milioni 200 za kufanyia usajili Manchester United
WANAOTAKIWA NA VAN GAAL...
KEVIN STROOTMAN 
Roma Pauni Milioni 25, miaka 24
2013-14 mechi: 28  mabao: 6
Anatumia mguu wa kushoto, mtaalamu, lakini hana kasi. Anasumbuliwa na maumivu goto na hataweza kuingia uwanjani hadi Oktoba.
CESC FABREGAS 
Barcelona Pauni Milioni 45, miaka 27
2013-14 Mechi: 55  Mabao: 13
Anauzwa. United inaweza kujaribu bahati yake.
TONI KROOS 
Bayern Munich Pauni Milioni 18, miaka 24
2013-14 Mechi: 51  Mabao: 4
Alikubali kujiunga na timu chini ya David Moyes. Van Gaal bado analitamani zao hilo la akademi ya Munich.
MATS HUMMELS 
Borussia Dortmund Pauni Milioni 20, miaka 25
2013-14 Mechi: 28  Mabao: 2
Hayuko fiti sana  lakini ni beki la kazi. Dortmund inaweza kumuuza
HOLGER BADSTUBER 
Bayern Munich Pauni Milioni 15, miaka 25
2013-14 Hajacheza mechi hata moja, lakini mbele ya van Gaal huyo ndiye beki bora zaidi anayetumia mguu wa kuhsoto ndani ya Ujerumani.
LUKE SHAW 
Southampton Pauni Milioni 27, miaka 18
2013-14 Mechi : 36  Hajafunga bao
Mchezaji huyo wa kimataifa wa England anaweza kujiunga na United mara sakata la ada ya uhamisho wake litakapomalizwa.
SEBASTIAN JUNG 
Eintracht Frankfurt Pauni Milioni 7, miaka 23
2013-14 Mechi: 36     Bao: 1
Beki wa kulia wa pili bora Ujerumani baada ya Philipp Lahm, ambaye Arsenal pia wanamtaka.

No comments:

Post a Comment