Kwisha habari yake: Cole, aliyeichezea mechi 107 England anastaafu soka la kimataifa
Huduma yake: Cole aliichezea England katika mechi yake ya kwanza dhidi ya Albania machi 2001.
ASHLEY
Cole ametangaza kustaafu soka la kimataifa baada ya kuachwa katika
kikosi cha timu ya Taifa ya England kinachoenda kushirki kombe la dunia
nchini Brazil kuanzia juni 12 hadi julai 13 mwaka huu.
Kocha wa England Roy Hodgson
amempigia simu beki huyo mwenye miaka 33 na aliyeichezea timu ya taifa
mechi 107 na kumueleza kuwa hatakuwepo katika kikosi chake na nafasi
yake imechukuliwa na beki wa Southampton, Luke Shaw.
Cole ameandika kwenye mtandao
wake wa Twita na kusema: “Nimepigiwa simu na Roy, tumekubaliana naye
kuwa timu ya England itakuwa na vijana. Nadhani ni muda muafaka wa
kustaafu kuchezea timu ya England sasa”.
“Tuna
kocha mkubwa na timu nzuri, nawatakia mafanikio mema. Nitawasapoti kama
shabiki wa kweli. Namshukuru kila mtu aliyenipenda na ambaye
hakunipenda, niamini, naumia sana kutolichezea taifa langu”.
Hodgson anatarajia kutangaza kikosi cha timu ya Taifa ya England leo majira ya saa 8:00 mchana.
No comments:
Post a Comment