SEVILLA
ya Hispania imetwaa ubingwa wa Europa League baada ya kuifunga Benfica
ya Ureno kwa penalti 4-2 kufuatia sare ya bila kufungana ndani ya dakika
120.
Mchezo
huo uliofanyika Uwanja wa Juventus, mjini Torino, Italia ulikuwa wa
kawaida na timu zote zilicheza kwa tahadhari, hali iliyosababisha hata
mashambulizi yawe machache.
Fainali kweli: Jose Antonio Reyes wa Sevilla akichuana na Rodrigo Moreno na Ruben Amorim wa Benfica katika Fainali ya Europa League usiku huu Uwanja wa Juventus mjini Torino.
Bacca,
M’Bia, Coke na Gameiro ndiyo walifunga penalti za Sevilla, wakati wa
Cardozo na Rodrigo walikosa za Benfica, huku Lima na Luisao wakifunga.
Sifa
zimuendee kipa Mreno wa Sevilla Antonio Alberto Bastos Pimparel
aliyewazuilia ndugu zake leo na kucheza penalti moja ya Rodrigo, wakati
ya Cardozo ilikwenda nje.
Ushindi
wa Sevilla unamaanisha mataji yote ya klabu ya UEFA msimu huu yamebaki
Hispania, kwani Atletico Madrid na Real Madrid nazo zitakutana katika
Fainali ya Ligi ya Mabingwa baadaye mwezi huu nchini Ureno.
Vikosi
vilikuwa, Sevilla: Beto, Coke, Pareja, Fazio, Moreno, Mbia, Carrico,
Reyes/Marin dk78/Gameiro dk104, Rakitic, Vitolo/Diogo Figueiras dk110 na
Bacca.
Benfica:
Oblak, Maxi Pereira, Luisao, Garay, Siqueira/Cardozo dk99, Ruben
Amorim, Gomes, Gaitan/Ivan Calvaleiro dk119, Sulejmani/Andre Almeida
dk25, Lima na Rodrigo.
![]() |
Wafalme; Wachezaji wa Sevilla wakiwa na taji la Europa League baada ya kuifunga kwa penalti Benfica |
Fainali kweli: Jose Antonio Reyes wa Sevilla akichuana na Rodrigo Moreno na Ruben Amorim wa Benfica katika Fainali ya Europa League usiku huu Uwanja wa Juventus mjini Torino.
Shujaa; Kipa Beto akipangua penalti ya Rodrigo |
No comments:
Post a Comment