Ikiwa
mwasiti ndio ametambulisha rasmi video yake hii ya Serebuka,
inayosifiwa na kila mtu jijini kwa jinsi ilivyokuwa na utofauti,
uliotokea kutokana na idea iliyotumika katika kufanyika kwa video hiyo
kali ya serebuka, mbali na uzuri wa video hiyo mengi yameanza kuongelewa
haswa kutokana na Linah akionekana kubusu picha ya aliyekuwa mpenzi
wake wa zamani Amini, huku watu kujiuliza ni nini haswa kinaendelea au
ndio kuserebuka kwenyewe.
Linah
na Amini walishawahi kuwa wapenzi, ila baada ya muda kila mmoja alikiri
kuwa wamebaki kuwa marafiki wakubwa tu, huku tetesi nyingine zikisikika
kuwa Linah ameshachukuliwa na mtu mwingine ambaye siyo Amini, hadi
ilipoonekana katika kipande cha video hiyo mpya ya Mwasiti, na kuacha
watu midomo wazi, kila mtu akijiuliza ni kweli itakuwa wamerudiana au ni
Sanaa tu iliyotumika katika kufikisha ujumbe katika video hiyo mpya
kali ya Mwasiti.
No comments:
Post a Comment