DUNIA ina mambo! Prizenta wa Radio Times FM, Hadija Shaibu ‘Dida’
amezua timbwili baada ya kung’ang’aniwa na mwanamke mwenzake aliyedaiwa
kutaka kumshawishi afanye naye mapenzi ya jinsi moja (usagaji).
Dida alikumbwa na ishu hiyo, Alhamisi ya wiki iliyopita ndani ya
Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni jijini Dar, wakati Kundi la Mashauzi
Classic, lilikuwa likiangusha burudani.
Katika tukio hilo
lililoshuhudiwa na ‘shushushu’ wetu, mwanamke huyo aliyetajwa kwa jina
moja la Addy ambaye anadaiwa kukubuhu kwa tabia hiyo chafu ya usagaji.
Ilisemekana kwamba mwanadada huyo alianza kumzengea Dida kwa kumsemesha huku akimuonesha pozi za kimahaba.
Licha ya mtangazaji huyo kumpuuza, Addy alifika mbali na kuanza
kumshtua kwa kutokea nyuma yake kwa kumtekenya huku akimkonyeza na
kumshawishi waongee vizuri.
Kutokana na vitendo hivyo, Dida
alipandwa na hasira na kuchukua chupa kutaka kumpasua ndipo Addy naye
akawa anahangaika kujitetea na kusababisha vurugu katika eneo hilo,
shukrani ziwaendee wasamaria wema waliwatuliza.
Akizungumza na Risasi Jumamosi mara baada ya kutulizwa, Dida alisema:
“Huyu dada ni muda mrefu alikuwa akinisumbua hapa ukumbini, mwanzo
nilikuwa sijajua anachotaka kumbe ni mshenzi kabisa, anataka kunifanya
vitendo vya kisagaji, amenikera sana.”
-GPL
No comments:
Post a Comment