Diamond Platnumz atazidi kuwa si msanii tu wa kawaida bali ni moja kati
ya wasanii wengi wa kimataifa.ukiacha pesa anayotoza treatment na
mahitaji yake hadi kumpandisha kupiga show moja si ya kitoto, kaa utulie
usikilize mahitaji haya ya Diamond: Kwanza bila kumtonyesha kuanzia
milioni 45 kwenda juu, utaishia kuongea naye kwenye simu tu, bila hata
ya kuona sura yake, achana na hiyo basi kwanza kama umeshatenga hilo
fungu na kufanikisha kumuita kupiga ku-sign contract yake, inabidi
umsafirishe kwa private jet au first class plane, akishatua uwe
umeshandaa presidential suit katika hoteli yeyote yenye
hadhi ya nyota tano, kama ni Bongo ni Serena hotel pale wakati huohuo
uwe umashatenga vyumba maalumu vikubwa kwa ajili ya team yake wakiwemo
Dancers,camera man,dj , mlinzi wake na msaidiz, microphone ya pekee na
vyakula atavyohitaji yeye, viwe teyari umeshaweka order vitengenezwe,
kama
anavyotaka yeye.
(U-ghari wa diamond unatokana na yeye mwenyewe kuwa brand kubwa,
anauwezo wa kujaza uwanja peke yake,lakin pia maandakiz ya kaz
zake,nyimbo ama video,hu-invest gharama kubwa,mfano number 1 video
orignal na rmx ilitumika zaidi ya million 80,lakin pia ana team
aliyowaajili anahitaj awalipe )
Kama ulikuwa unamchukulia Dangote easy, jipange!.
No comments:
Post a Comment