Friday, 16 May 2014

ETO'O AMBATIZA MOURINHO 'MPUMBAVU'...NA ASEMA ATAENDELEA KUCHEZA LIGI YA MABINGWA

MSHAMBULIAJI Samuel Eto'o ameripotiwa kukana madai kwamba yupo karibu kustaafu baada ya kumuita kocha wake, Jose Mourinho ni 'mpumbavu' kwa kuhoji umri wake.
Mwanasoka huyo mwenye umri wa miaka 33 ilivumishwa amekorofishana na Mourinho baada ya kocha huyo wa Chelsea kuchukuliwa na Televisheni ya Ufaransa akisema; "Eto’o ana miaka 32, labda 35, nani anajua?".
Pamoja na hayo Eto'o alionyesha kuchekeshwa na maelezo hayo na kuigiza kushangilia kama kikongwe akitumia mkongojo baada ya kufunga boa dhidi ya Manchester United Januari, yakiwa ni majibu kwa kocha huyo Mreno.
Majibu tosha: Samuel Eto'o alifanya hive kushangilia kama kikongwe akipeleka majibu kwa Jose Mourinho aliyehoji umri wake

Akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kutua Abidjan kwa ajili ya michuano ya vijana ya Copa Coca Cola michuano inayofanyika mjini Bouake, Eto'o alisema: "Nina umri wa miaka 33. Na si kwa sababu mpumbavu ameniita mzee basi unatakiwa kuamini. "Na unatakiwa kujua kwamba, mzee alikuwa bora kuliko nyota chipukizi,".
Eto'o, sass amemaliza Mkataba wake baada ya msimu huu The Blues, pia amesema kwamba ni bora angeendelea kucheza klabu ya Ulaya kuliko kwendea Mashariki ya kati kwa mkataba mnono.
"Baadhi wanaamini nitakwenda kustaafu Marekani au Mashariki ya Kati, lakini nimerudiaa furaha ya kucheza Ligi ya Mabingwa na nitaendelea kucheza Ligi ya Mabingwa,".
In doubt: Chelsea boss Mourinho was filmed questioning Eto'o's age
Ana shaka: Kocha wa Chelsea, Mourinho alikaririwa akihoji umri wa Eto'o

"Wapi? Sitakuambia. Lakini nitaendelea kucheza, kwa sababu kiakili na kimwili bado niko vizuri. Hivyo, ninakwenda kwenye Kombe hili la Dunia na lingine pia wakati nitakapokuwa na umri wa miaka 37. Wengine wamefanya hivi wakiwa na umri wa miaka 42, hivyo ninaweza kucheza kwenye fainali mbili zaidi za Kombe lka Dunia,"alisema.
Veteran: Eto'o will take part in his fourth World Cup with Cameroon in Brazil this summer
Mkongwe: Eto'o atacheza fainali za Nne za Kombe la Dunia mwaka huu nchini Brazil

No comments:

Post a Comment