Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uratibu na Uhusiano), Stephen Wassira
amewatisha wabunge wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kwamba
wasiporejea bungeni, kanuni zitabadilishwa na Bunge litaendelea.
Wassira alitoa kauli hiyo bungeni jana wakati akijibu hoja za wabunge
mbalimbali akiwamo Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee kuwa
majadiliano ndani ya Bunge la Katiba yanakiuka Sheria ya Mabadiliko ya
Katiba.
Katika mchango wake, Mdee alisema Ukawa hawako tayari kurejea ndani ya
Bunge Maalumu la Katiba Agosti, mwaka huu endapo majadiliano ya Katiba
hiyo hayatajikita kwenye Rasimu ya Pili ya Katiba.
Hata hivyo, Wassira akijibu kauli hiyo ya Mdee na wabunge wengine
waliopaza sauti kuhusu kukiukwa kwa sheria hiyo alisema: “Kama hamrudi
tutatumia kanuni zile kutafuta akidi na Bunge litaendelea.”
“Tusigeuze Bunge hili kuwa Bunge la Katiba… Bunge la Katiba lipo tena
lipo kisheria…. Kuna watu wanageukageuka wanasema sheria ilivunjwa,
lakini hawasemi kifungu gani kilivunjwa,” alisema Wassira.
Wassira alisema wajumbe wa Bunge la Katiba walitunga Kanuni za Bunge
hilo na miongoni mwa waliokuwa walimu wa kanuni hizo alikuwa Ismail
Jussa na Tundu Lissu ambao ni wajumbe wa Ukawa.
“Kanuni tuliyotunga ambayo haipingani na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba
ni Bunge hilo kuwa na mamlaka ya kubadili, kurekebisha, kuboresha na
kadhalika,” alisema Wassira na kuongeza:
No comments:
Post a Comment