Diego Costa akiwa mjini Belgrade kwa lengo la kuonana na mganga wa kienyeji.
MSHAMBULIAJI
wa Atletico Madrid, Diego Costa amesafiri kwenda Belgrade nchini Serbia
kumuona `Mganga wa miujiza`, Marijana Kovacevic ili amtibu na kurejea
uwanjani haraka kwa ajili mchezo mkubwa zaidi katika maisha yake ya
soka.Mganga huyo wa Serbia anawatibu
wachezaji wenye matatizo ya misuli kwa kuwawekea placenta na Costa
anataka kuichezea Atletico Madrid kwenye mechi ya fainali ya UEFA dhidi
ya Real Madrid jumamosi ya wiki hii.
Costa amekuwa akisumbuliwa na
majeruhi ya nyama aliyopata wiki iliyopita kwenye mechi ya mwisho ya
ligi kuu nchini Hispania, La Liga dhidi ya FC Barcelona iliyomalizika
kwa sare ya 1-1 na Atletico kufanikiwa kutwaa ubingwa.
Diego Costa amesafiri kwenda Belgrade kuonana na mganga wa miujiza, Marijana Kovacevic
Costa (katikati) yuko hatarini kukosa mechi ya fainali ya UEFA dhidi ya Real Madrid.
![](http://i.dailymail.co.uk/i/pix/2014/05/20/video-undefined-1E0A864500000578-32_636x358.jpg)
Majeruhi
aliyonayo Costa kwa sasa siku zote humfanya mchezaji akae nje ya uwanja
kwa siku 15 na kama hatapata nafuu, basi atakosa mechi ya Lisbon.
Kovacevic
aliwahi kuwatibu wachezaji wengi wa ligi kuu akiwemo mshambuliaji wa
zamani wa Asernal Robin van Persie na kiungo wa Chelsea, Frank
Lampard.
No comments:
Post a Comment